WIKI ILIYOPITA WANA CLOUDS FM NA CLOUDS TV WALISHEREHEKEA SIKU YA KUZALIWA YA MFANYAKAZI MWENZAO Hellen Kazimoto-Pata Vituko Vyao-My Role Models

By Gadiola Emanuel - 11:13:00 AM


Anaitwa Hellen Kazimoto yeye yupo kitengo cha events mbalimbali za clouds fm na clouds tv kama mratibu.Birthday yake ilikuwa tarehe 7 October ijumaa iliyopita.Aliamua kuifanyia katika ufukwe wa coco beach tukakutana marafiki zake kibao pande zile.

Hellen Kazimoto ,Dina Marios , Arnold Kayanda(mzee wa Jahazi).Kulikuwa na kired carpet cha kizushi kwa ajili ya kupiga picha.
Aisha,Adam,Hellen na Junior.

B12(My role Model),Hellen na Dj Fetty


Mwanamuziki Alpha na Doreen wakiwakilisha ki roho safi.

Millard Ayo,Hellen,Moonshine,Arnold.

Mwanamuziki Bob Junior na Hellen

Kulikuwa na jiko hapo ni mishikaki,kuku na mbuzi choma.

Kuna mchezo siku hizi umeenea yaani ikiwa ni siku yako ya kuzaliwa watu wanachofanya ni kukumwagia maji tu.Kama umeifanyia nyumbani ndio balaa watu wanakaa na ndoo za maji wanakuvizia umejisahau tu mwaaaaaaaaaa unamwagiwa.Sasa bibi huyu kwa sababu sherehe ilikuwa ufukweni ndio kubebwa mpaka baharini.

Wakamuweka humo kwenye maji....mambo gani haya!!!!Nasema kabisa mimi ntakodi baunsa wale wenye mbavu nene mwili nyumba atakae nimwagia maji anabebwa juuu juuu na kutolewa nje ya eneo la tukio.

Haya bibi huyo akarudi amelowa chapachapa mpaka nguo ya ndani... Ikabidi abadilishe nguo na kupata picha na Balozi.



Heeee ikafika wakati wa kufungua champaign si nayo wakaanza kumwagia..hawa watoto kama wamerogwa!!

Huyu Arnold anakihere here sana sasa ngoja bday yake mwezi wa kumi na mbili atajutaje?

Ukafika wakati wa kukata keki na kuimba happy birthday to dear Hellen..keki ikakatwa!


Dina Marios huyooooo Ikafika zamu yake ya  kula keki, heeeeeee kumbe kuna mchezo mwingine ukila keki ile cream ya keki unapakwa usoni jamaniiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!!!

Dahhhhhhhh yaani kwenda kunawa uso tena haya sawa ntafanyaje ndio style ya kusherehekea.

Adam Mchomvu hahahahahahahahahahaha!alijutaje


Basi mziki ukaendelea na duara likazungushwa pale kati ikawa ni mambo ya kachiriii kachiriiii saga...


Mwasiti aliyechuchumaa na marafiki

Watu kibaooo katika picha ya pamoja ukiangalia vizuri utatujua..


Mwisho wa party kiukweli ilikuwa nzuri na tukawa tumekula ma gud time.Nilipenda wazo la kufanya bday party ufukweni usiku mzito tukarudi makwetu.
Picha na Dina Marios Blog

  • Share:

You Might Also Like

0 comments