MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AHUDHURIA SHEREHE ZA KUMBUKUMBU YA KIFO CHA SAMORA MACHEL-MAPUTO
By Gadiola Emanuel - 12:36:00 PM
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akisalimiana na aliyekuwa mke wa Rais wa zamani wa Mozambiq,
Mama Graca Machel, wakati walipokutana na katika viwanja vya Mozambiq
Heroes Square, kwenye sherehe za maadhimisho ya Kumbukumbu ya kifo cha
mwasisi wa nchi hiyo, Samora Machel, zilizofanyika leo Oktoba 19, mjini
Maputo. Kulia kwa Makamu ni Mama Zakhia Bilal na (katikati) ni Rais wa
Afrika ya Kusini, Jacob Zuma. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Mama
Maria Nyerere akiweka Shada la Maua ndani chumba maalum mahala lilipo
kaburi la mwasisi wan chi ya Mozambiq, wakati wa maadhimisho ya sherehe
za kumbukumbu ya kifo cha mwasisi huyo zilizofanyika mjini Maputo
Msumbiji leo Oktoba 19.
Makamu wa Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib
Bilal, akiteta jambo na Rais wa Afrika ya Kusini, Jacob Zuma, wakati
walipokutana na katika viwanja vya Mozambiq Heroes Square, kwenye
sherehe za maadhimisho ya Kumbukumbu ya kifo cha mwasisi wa nchi hiyo,
Samora Machel, zilizofanyika leo Oktoba 19, mjini Maputo. Kulia kwa
Makamu ni Mama Zakhia Bilal na (katikati) ni Rais wa Afrika ya Kusini,
Jacob Zuma.
Kingunge Ngombale Mwilu, akijumuika na wananchi wa nchini Mozambiq,
kuelekea kuweka mashada ya maua katika kaburi la Mwasisi wa nchini hiyo,
wakati wa sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa
rais wan chi hiyo, Samora Machel, zilizofanyika leo Oktoba 19.
Askari
wakimuongoza Rais wa Mozambiq, Armando Guebuza, kuelekea kuweka Shada
la maua katika Kaburi la Mwasisi wan chi hiyo, ambaye pia aliwahi kuwa
Rais wa nchini hiyo, Samora Machel, wakati wa sherehe za maadhimisho ya
Kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Mwasisi na Rais wa Mozambiq, Samora
Machel, zilizofanyika leo Oktoba 19 mjini Maputo Msumbiji.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal,mkewe Mama Zakhia Bilal na Mama Maria Nyerere,wakiwa pamoja na
baadhi ya Marais wan chi za Afrika wakati walipohudhulia katika sherehe
za maadhimisho ya Kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Mwasisi na Rais wa
Mozambiq, Samora Machel, zilizofanyika leo Oktoba 19 mjini Maputo
Msumbiji.
Picha na Muhidin Sufiani-OMR
0 comments