KONGAMANO LA WANAHABARI LA BIMA YA AFYA MORO

By Gadiola Emanuel - 6:24:00 AM

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (kulia), akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari,baada ya kufungua kongamano la saba la mwaka la wahariri wa habari na waandishi waandamizi la kujadili taarifa za utafiti wa huduma za NHIF nchini. Kongamano hilo la siku mbili lilianza jana mjini Morogoro.
Wachora vibonzo Nathan Mpangala (kulia) na King Kinya wakisikiliza kwa makini wakati wa kongamano likiendelea.
Baadhi ya wahariri wa habari na waandishi waandamizi wakiwa katika kongamano la saba la mwaka la kujadili taarifa za utafiti wa huduma za NHIF nchini, lililoanza jana mjini Morogoro.
Beda Msimbe wa magazeti ya Serikali ya Daily News na Habari Leo, akitoa taarifa ya utafiti wa huduma zitolewazo na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), katika Mkoa wa Ruvuma.
Mwandishi wa Habari, Joshua Joel wa ITV Sumbawanga akifafanua jambo alipokuwa akitoa katika kongamano hilo taarifa ya utafiti wa upatikanaji wa huduma za afya zitolewazo na NHIF, katika mikoa ya Rukwa na Katavi.

  • Share:

You Might Also Like

0 comments