UFUNGUZI WA MKUTANO WA UWEKEZAJI MJINI MPANDA LEO

By Gadiola Emanuel - 10:41:00 AM

Rais Jakaya Kikwete akifungua mkutano wa uwekezaji katika ukanda wa ziwa Tanganyika mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Idara ya maji mjini Mpanda ukishirikisha Mabalozi. Mwaziri, Maafisa wa Serikali, Wafanyabiashara, na wawekezaji wa nje na ndani ya nchi Mkutano huo umepewa jina na (Lake Tanganyika Zone Investment Forum), Katika picha kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injini Stella Manyanya na katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mabalozi mbalimbali mara baada ya kufungua rasmi mkutano huo leo mjini Mpanda.
Rais Jakaya Kikwete akiuzindua rasmi mtandao wa utakaoshughulikia taarifa na habari mbalimbali za uwekezaji katika ukanda wa ziwa Tanganyika huku Waziri Mkuu Mizengo Pinda wa pili kutoka kulia akishuhudia, kulia kwa Rais ni Mkuu wa mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya na kulia ni Dk. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dr Mary Nagu.
Rais Dk. Jakaya Kikwete akiwahutubia wageni waalikwa mbalimbali katika mkutano huo.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi mbalimbali waliohudhuria katika mkutano huo.

Picha na Full Shangwe Blog

  • Share:

You Might Also Like

0 comments