Mashindano ya baiskeli Vodacom Mwanza Open Cycle Challenge yarindima jijini Mwanza...ARUSHA YATISHAA
By Gadiola Emanuel - 1:14:00 PM
Hatimaye
Richard Laizer wa mkoani wa Arusha ndiye ametegua kitendawili cha
nani anayepaswa kuwa mshindi wa mbio za wazi za baiskeli za Vodacom
Mwanza Open Cycle Challenge baada ya kuwashinda washiriki wengine
zaidi ya 400 walijitokeza kushiriki kwenye mashindano hayo kwa upande
wa wanaume.
Hapa
mshindi huyo wa mbio za Mwanza Open Vodacom Cycle Challenge 2011
kutoka klabu ya Arusha Cycling Richard Laizer akipokea zawadi yake ya
shilingi milioni 1.500.000 kutoka kwa Mkuu wa Udhamini wa Kampuni ya
Vodacom Tanzania George Rwehumbiza mara baada ya kutajwa katika mbio
hizo za kilomita 196 zilizoanzia Busanda mkoani Shinyanga na
kumalizikia Bugando Hills jijini Mwanza.
Picha
kulia ni Steven Kingu Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Kanda ya Ziwa na
kulia kwa George Rwehumbiza ni Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya bia
ya Serengeti SBL. Mdhamini mkuu wa mashiundano hayo ni kampuni ya simu
za mkononi ya Vodacom ikishirikiana na wadhamini wenza kampuni ya bia
ya Serengeti SBL na Kituo cha Radio cha Clouds Fm.
Richard
Laizer wa mkoani wa Arusha ndiye akionyesha zawadi zake mara baada ya
kukabidhiwa rasmi jioni ya leo kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini
Mwanza.
Morris
Njowoka Meneja wa kinywaji cha Malta Guinness akimkabidhi zawadi mmoja
wa washindi wa wa mbio za baiskeli za Vodacom Mwanza Open Cycle
Challenge.
Mkurugenzi
wa Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti SBL Ephraim Mafuru
akikabidhi zawadi kwa Zavalina Abel aliyeshiriki katika mbio za
kilomita 10.
Wadau
wakipozi kwa picha kutoka kulia ni G. Sengo wa Clouds Mwana, Amicus
Butunga wa TBC Mwanza, mkuu wa kambi John Bukuku (Mzee wa Full Shangwe blog) na mwisho ni Moriss
Njowoka Meneja wa kinywaji cha Malta Guiness. Hii
ndiyo timu ya Arusha Cycling iliyofanya vizuri kwa uoanda wa wanawake
na wanaume kama unavyowaona na wamependeza kweli kwa vivazi vyao.
Mkurugenzi
wa masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti SBL Ephraim Mafuru
akimpongeza Sophia Husein kutoka klabu ya Arusha Cycling aliyeshinda
kilomita 80 wanawake baada ya kupokea zawadi zake kulia ni Moriss
Njowoka Meneja wa kinywaji cha Malta Guiness..
Richard Laizer wa mkoani wa Arusha akipongezwa na mashabiki wake mara
baada ya kumaliza mashindano hayo katika vilima vya Hospitali ya
Bugando jijini Mwanza.
Mkurugenzi
wa masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti SBL Ephraim Mafuru
akijadiliana jambo na Stanslaus Mbaga Mkuu wa Masoko Kanda ya Ziwa na
Anold Kileo Meneja wa matangazo.
M ashabiki mbalimbali wakiwa katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakishuhudia utoajiwa zawadi kwa washindi.
0 comments