WAZIRI KOMBANI, JAJI WEREMA WAITWA MBELE YA KAMATI YA BUNGE YA KATIBA, SHERIA NA UTAWALA LEO

By Gadiola Emanuel - 7:45:00 AM


Waziri wa katiba na Sheria Mhe. Celina Kombani akifafanua Jambo Mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge Katiba, Sheria na Utawala mara baada ya Kuwasilisha baadhi ya mabadiliko katika Muswada huo yaliyoletwa na Serikali. Kamati hiyo ndiyo inayoshughulikia Muswada wa Mabadiliko ya Katiba, kabla haujawasilishwa Bungeni.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema akifafanua mbele ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala baadhi ya vifungu vilivyomo katika Muswada wa Mabadiliko ya Katiba, ambao unashughulikiwa na kamati hiyo kabla haujawasilishwa Bungeni. Waziri wa katiba na Sheria Mhe. Celina Kombani na Mwanasheria Mkuu wa Serikali waliitwa mbele ya Kamati leo kufafanua baadhi ya vifungu katika muswada huo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Katiba, Sheria na Utawala Mhe. Pindi Chana (Mb) akishauriana Jambo la kikanuni na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Angela Kairuki (Mb), mara baada ya kupokea ufafanuzi wa kutoka kwa Waziri wa katiba na Sheria Mhe. Celina Kombani (Kulia) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema (hayupo Pichani) ambao waliitwa mbele ya Kamati leo kufafanua baadhi ya vifungu katika muswada wa Mabadiliko ya Katiba.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Katiba, Sheria na Utawala wakifuatilia maelezo kutoka kwa Waziri wa katiba na Sheria Mhe. Celina Kombani (Mb) aliyeitwa mbele ya kamati kutoa maelezo kuhusu Maboresho katika Muswada wa Mabadiliko ya katiba. Kamati hiyo ha Bunge iliwaita Waziri wa katiba na Sheria Mhe. Celina Kombani (Mb) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema kufafanua baadhi ya vifungu katika muswada wa Mabadiliko ya Katiba. 
Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge.

  • Share:

You Might Also Like

0 comments