Madaktari watekwa nyara huko Kenya,mpakani na Somalia

By Gadiola Emanuel - 11:32:00 AM

Daadab
Kambi ya Daadab
 Watu wenye silaha wamewateka nyara madaktari wawili wa Uhispania wanaofanya kazi na shirika la misaada la Medicins Sans Frontiers (MSF) karibu na mpaka na Somalia nchini Kenya.
Wawili hao walitekwa katika kambi ya wakimbizi ya Daadab, ambayo inawahifadhi maelfu ya wakimbizi wanaokimbia njaa katika Pembe ya Afrika.
Dereva wao, raia wa Kenya, alijeruhiwa na sasa amepelekwa hospitali, limesema shirika la MSF.
Katika wiki za hivi karibuni, wanawake wawili, mmoja raia wa Uingereza na mwingine Mfaransa walitekwa karibu na mpaka huo.
Polisi wa Kenya wameiambia BBC kuwa wanawafuatilia watekaji nyara hao kwa kutumia magari na ndege.
MSF imethibitisha kupotea kwa madaktari wake raia wa Ulaya wawili, na wametoa taafifa fupi.
"Asubuhi ya leo wafanyakazi wa MSF walipatwa na tatizo huko Daadab" imesema taarifa hiyo.
"Dereva mmoja amejeruhiwa: Kwa sasa hyuko hospitali na hali yake sio mbaya. Wafanyakazi wawili wa kimataifa hawajulikani walipo. Kikosi chetu cha dharura kimeundwa kukabiliana na tatizo hili.
Shambulio hilo limetokea katika kam,mbi ya Ifo, moja ya maeneo yanayounda Daadab, takriban kilomita 80 kutoka mpaka na Somalia. Kwa ujumla Daadab sasa inahifadhi wakimbizi 450,000, na kulifanya eneo hilo kuwa kama jiji la tatu kwa ukubwa nchini Kenya.
Mwandishi wa BBC nchini Kenya amesema dereva alipigwa risasi mara kadhaa shingoni na hali yake si nzuri sana na amelazwa hospitali.

Mwezi uliopita, raia mmoja wa Uingereza Judith Tebutt (56) alitekwa nyara na watu wenye silaha kutoka katika hoteli iliyopo Kiwayu. Mume wa mwanamke huyo David, aliuawa. Bibi Tebbutt anaaminiwa kuwa anashikiliwa na kundi la al-Shabaab nchini Somalia.


Tarehe mosi Oktoba, mwanamama mwingine raia wa Ufaransa alitekwa na kundi la watu wenye silaha katika kisiwa cha Manda nchini Kenya na kupelekwa Somalia.

Dereva mmoja raia wa Kenya anayefanya kazi na shirika la Care alitekwa nyara kutoka Daadab Septemba 21.

na BBC habari

  • Share:

You Might Also Like

0 comments