NBC yaandaa tafrija kwa wadau na wanachama wa Mfuko wa PPF

By Gadiola Emanuel - 9:10:00 AM

Mkuu wa Mauzo Kitengo cha Makampuni wa NBC, Bi. Minnie Kibuta (kushoto) akimpakuliaji chakula Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Mashirika ya Umma (PPF) William Erio katika hafla iliyoandaliwa na NBC kwa wadau na wanachama wa PPF waliokuwa katika mkutano wao jijini Arusha mwishoni mwa wiki.
Mshauri wa Mambo ya Habari wa NBC, Redemptus Masanja (kushoto) Ofisa Uhusiano, Eddie Mhina na mdau wa PPF Muhidini Michuzi wa Globu ya Jamii wakibadilishana mawazo katika hafla hiyo mjini Arusha mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Mauzo Kitengo cha Makampuni wa NBC, Bi. Minnie Kibuta akizungumza katika hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na NBC kwa wadau wa PPF mjini Arusha mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Mashirika ya Umma (PPF) William Erio (kulia) akisalimiana na Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, Bi. Robi Matiko , wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki hiyo kwa wanachama na wadau waliokuwa wakihudhuria Mkutano Mkuu wa 21 wa PPF jijini Arusha mwishoni mwa wiki. Katikati ni Meneja Mahusiano wa PPF, Bi. Lulu Melenge.
Baadhi ya wadau wa PPF wakifujadiliana mambo mbalimbali na kuota moto katika hafla hiyo pembeni mwa jiko la moto lililowekwa kwa ajili ya hali ya hewa ya kibaridi iliyopo mjini Arusha kwa sasa.
Kikundi cha wamasai kikitoa burudani katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Mashirika ya Umma William Erio (katikati) akisalimiana na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC, Mwinda Kiula-Mfugale wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki hiyo kwa wanachama na wadau waliokuwa wakihudhuria Mkutano Mkuu wa 21 wa PPF jijini Arusha mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkuu wa Mauzo Kitengo cha Makampuni, Minnie Kibuta.
na Fullshangwe blog 

  • Share:

You Might Also Like

0 comments