WAZIRI NCHIMBI AZINDUA SHEREHE ZA JANDO KWA VIJANA WA KIMASAI

By Gadiola Emanuel - 2:38:00 PM


WAZIRI wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Emanuel Nchimbi akivalishwa shuka la kimasai kwa ajili ya kupewa shukurani ya kwenda kwenye sherehe hizo.

waigizaji wa kikundi cha sekei youth group wakiwa wanaonyesha igizo.

WAZIRI wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Emanuel Nchimbi ametaka
Watanzania kuzingatia maadili yatokanayo na Mila na desturi ikiwa ni
pamoja na kudumisha mila zao.
Waziri huyo alisema kuwa ikiwa Watanzania wataweza kudumisha mila na
desturi zao hali hiyo itasaidia kuongezeka kwa maadili hususani kwa
vijana ambao kwa hivi sasa maadili yamepungua kwa kiasi kikubwa.
Nchimbi alitoa rai hiyo jana katika kata ya Enaboishu iliyopo wilayani
Arumeru mkoani hapa wakati alipokuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa
sherehe za jando kwa vijana wa kiume wa rika la "Ilkishiru" zoezi
lililoanza jana.
Alisema kuwa hapa nchini makabila mengi yamepuuza mila na desturi zao
ambapo alisema kwua Wamasai wanaongoza kwa kufuata na kutunza mila
zao.
Aliyataka makabila mengine hapa nchini kuiga mfano huo wa wamasai kwa
kuendeleza tamaduni zao kwa vizazi vyao na vijavyo.
"Utamaduni huu wa kudumisha mila unatakiwa kuigwa na makabila mengine kwani tabia ya vijana kutojali na kutokuheshimu wazazi na wakubwa hao umekithitri hapa nchini hivyo kupitia mila na desturi hizo maadili yaliyoporomoka yatanogezeka"alisema 

Alisema kuwa kwa mila zao Rika hupishana kila baada ya miaka 14 ambapo
zoezi hilo hufanyika,ambapo pia waliipongeza serikali kwa kudumisah
mila na desturi.
Pia waziri huyo alijitolea kumsomesha kijana mmoja mwenye umri wa miaka saba aliyejulikana kwa jina la Edward Losanye mkazi wa Olkolada,mwafunzi wa shule ya msingi Enguita anayesoma darasa la tano ambaye ndio kijana mdogo kuliko wate ambaye anapelekwa jando
"mimi najitolea kumsomesha huyu mtoto kuanza hapa alipo mpaka sekondari kwakuwa ndio kina mdogo anayejiamini na ameamua kwenda jando akiwa mdogo Tanzania tunaitaji vijana wakaka mavu na majasiri kama hawa amenifurahisha sana"Alisema

Waziri wa habari vijana utamaduni na michezo Emanuel Nchimbi akiwa na mwenyeji wake naibu waziri wa aridhi nyumba maendeleo na makazi Godluck Ole Medeye wakiwa wanajadili jambo .
Waziri wa habari  vijana utamaduni na michezo Emanuel Nchimbi akiwa na mwenyeji wake naibu waziri wa aridhi nyumba maendeleo na makazi Godluck Ole Medeye wakiwa wanawasili kwenye sherehe za uzinduzi wa sherehe za jando kwa vijana wa kimaasai.

  • Share:

You Might Also Like

0 comments