Airtel yafunika tamasha la Miaka 50 ya Uhuru wa Kuongea huko Mbeya

By Gadiola Emanuel - 11:46:00 AM

Msanii wa Vichekesho King Majuto akiwa na mchekeshaji nwenzake wakionesha vituko vyao jukwaani wakati wa tamasha la burudani la miaka 50 ya Uhuru wa Kuongea lililoandaliwa na Kampuni ya simu ya Mkononi ya Airtel na kufanyika katika viwanja vya Luandanzove mjini Mbeya mwishoni mwa wiki, airtel pia ilisherehekea uzinduzi rasmi wa minara 20 katika vijiji ishirini ili kutoa mawasiliano bora mkoani mbeya.
 Mzee King Majuto akiwa katika kundi la watoto
Msanii wa muziki wa kizazi kipya wa Bongo Fleva Barnaba Boy kutoka kundi la THT akitumbuiza mamia ya wakazi wa mji wa Mbeya na vitongoji vyake wakati wa tamasha la burudani la miaka 50 ya Uhuru wa Kuongea.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya wa Bongo Fleva Juma Nature  akitumbuiza mamia ya wakazi wa mji wa Mbeya na vitongoji vyake wakati wa tamasha la burudani la miaka 50 ya Uhuru wa Kuongea lililoandaliwa na Kampuni ya simu ya Mkononi ya Airtel na kufanyika katika viwanja vya Luandanzove mjini Mbeya mwishoni mwa wiki.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya wa Bongo Fleva Roma akitumbuiza mamia ya wakazi wa mji wa Mbeya na vitongoji vyake wakati wa tamasha la burudani la miaka 50 ya Uhuru wa Kuongea.
picha na Father Kidevu blog

  • Share:

You Might Also Like

0 comments