MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemfutia
mashitaka mawili ya ugaidi, Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Bw. Wilfred Lwakatare.
Jaji
aliyekuwa akiendesha shauri hilo, Lawrence Kiduri, amemfutia Lwakatare
mashitaka hayo na kumbakizia kosa la kujaribu kumwekea sumu, Mhariri wa
gazeti la Mwananchi, Dennis Msaki, ambalo dhamana yake iko wazi.
Akizungumza
na GPL, wakili wa mshitakiwa huyo, Peter Kibatara, amesema wanatarajia
kumtoa kwa dhamana mteja wake huyo siku ya Jumatatu ambayo anaamini kuwa
taratibu zote zitakuwa zimekamilishwa.
Lwakatare akimkumbatia kwa furaha wakili wake, Peter Kibatara, baada ya kufutiwa mashitaka ya ugaidi.
Askari wakimuamuru Lwakatare kuondoka kizimbani kwa ajili ya safari ya gerezani.
Akiwaonyesha wafuasi wake alama ya ushindi wa chama chao.
Ulinzi ndani ya mahakama.
Ndugu, jamaa na wafuasi wa Chadema wakikumbatiana kwa furaha.
Mmoja wa wanachama wa Chadema akiwapigia simu wenzake kuwapasha kilichojiri mahakamani.
Ulinzi nje ya jengo la mahakama.
Wafuasi wa Chadema wakitoka mahakamani kwa furaha.
Kibatara akifafanua jambo kutoka kwenye makabrasha yake
Lwakatare akirudishwa rumande kwa kosa moja la kutaka kumwekea sumu, Dennis Msaki.Source Arusha 255
0 comments