MHE. MIZENGO PINDA ATEMBELEA KANISA LA OLASITI ,JIJINI ARUSHA

By Gadiola Emanuel - 2:17:00 AM

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Viongozi na Waumini wa Kanisa Katoliki la Olasiti Jijini Arusha alikokwenda kutoa pole kufuatia mlipuko wa bomu la kutupwa kwa mkono uliotokea kanisani na kusababisha vifo na majeruhi.
Paroko wa Kanisa Katoliki la Olasiti la Arusha Peddy Castelino akiomba wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipotembelea kanisa hilo na kutoa pole kufuatia mlipuko wa bomu la kutupwa kwa mkono uliotokea kanisani hapo May 5,2013 na kusabisha vifo na majeruhi.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Paroko wa Kanisa Katoliki la Olasiti jijini Arusha, Peddy Castelino (kulia)  wakati alipotembelea kanisa hilo May 5,2013 ambako ulitokea mlipuko wa bomu la kutupwa kwa mkono na kusababisha vifo na majeruhi.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiangalia sehemu lilipodondoshwa bomu hilo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapa Pole Askofu wa Jimbo Kuu la Arusha, Mhashamu Josephat Lebulu (kushoto ) na Balozi wa Vatican nchini, Askofu Mkuu, Francisco Montecillo (katikati), baada ya kutembelea Kanisa Katoliki la Olasiti jijini Arusha ambako May 5,2013 ulitokea mlipuko wa bomu la kutupwa kwa mkono na kusababisha vifo na majeruhi.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

  • Share:

You Might Also Like

0 comments