MAZISHI YA WALIOKUFA KWA BOMU LILILOLIPUKA KATIKA KANISA LA MT. JOSEPH OLASITI ,JIJINI ARUSHA
By Gadiola Emanuel - 5:28:00 AM
Maaskofu
wakiombea miili ya marehemu Regina Loning'o Laizer ,James Gabriel Kessy
na patricia Assey kabla ya kuingizwa kanisani tayari kwa ibada ya
mazishi iliyofanyika katika kanisa la mtakatifu josephy mfanyakazi
lililopo katika kata ya olasiti mjini hapa ambapo marehemu hawa ambao
walifariki dunia may 5 wakati wakisali katika ibada ya uzinduzi wa
kanisa ambapo mtu asiyejulikana alirusha bomu wamezikwa nje ya kanisa
hilo. Picha hii imepigwa na Woinde Shizza
Majeneza yakiwa kanisani kabla ya ibada ya mazishi
Mapadri wakiwa wamebeba moja ya majeneza
Watawa wakiwa kanisani wakati wa ibada
Viongozi wa Kanisa wakitoa salamu za mwisho
Kilio kilio kilio anamlilia mama yake mzazi
Wananchi wakitoa salamu zao za mwisho kwenye kanisa katoliki.
Majonzi na uchungu
Wahudumu
wakishusha mwili wa marehemu kaburini kwenye viwanja vya Kanisa la
Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Parokia ya Olasiti jijini Arusha.
Baadhi ya maaskofu kutoka majimbo mbalimbali waliohudhuria ibada ya mazishi.
Mkuu
wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania(KKKT)Dk Alex
Malasusa(kushoto)akiwa na viongozi wengine wa Kanis a hilo wakiwa kwenye
ibada ya mazishi
Umati wa watu waliohudhuria maziko hayo
Waziri
Mkuu mstaafu,Edward Lowassa(kulia)akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya
Ndani,Dk Emmanuel Nchimbi kabla ya ibada kuanza. Kuanzia picha ya pili: Filbert Rweyemamu
Waziri wa Mambo ya ndani, Dk Emmanuel Nchimbi akiweka shada la maua kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliyeondoka kabla ya zoezi hilo kufanyika, katika ibada ya mazishi ya waumini waliokufa baada ya kulipuliwa na blomu katika Kanisa la Katoliki la Mt Josephat Mfanyakazi – Parokia ya Olasiti, Arusha.
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe akiweka shada la maua katika moja ya makaburi hayo.
Majeneza yenye miili ya marehemu ikiwa kanisani tayari kuombewa. Marehemu hawa walifariki katika mlipuko wa bomu katika Kanisa la Mt Josephat Mfanyakazi – Parokia ya Olasiti, Arusha wakati ibada ikiwa ineendelea.
PICHA KWA HISANI YA SEIF MANGWANGI, FILBERT RWEYEMAMU NA WOINDE SHIZZA
0 comments