DR. JAKAYA KIKWETE AKIHANI MISIBA YA WALIOKUFA NA BOMU

By Gadiola Emanuel - 2:40:00 AM



Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakihani msiba wa marehemu Regina Longino Kurusei (45), mkazi wa Olasiti aliyefariiki katika shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti jijini Arusha Jumapili iliyopita.
Mama Salma Kikwete akipungia wakati msafara wa Rais Kikwete ukiondoka baada ya kuhani msiba wa msichana Patricia Joachim Assey (10) katika kitongoji cha Majengo kata ya Elerai aliyefariki kutokana na mlipuko wa bomu Jumapili iliyopita katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti. katika kitongoji cha Majengo kata ya Elerai jijini Arusha.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakihani msiba wa  msichana Patricia Joachim Assey (10) nyumbani kwa wazazi wa marehemu  katika kitongoji cha Majengo kata ya Elerai aliyefariki kutokana na  mlipuko wa bomu jumapili iliyopita Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia
ya Olasiti, jijini Arusha.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakishiriki dua ya pamoja, wakati walipomtembelea Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Askofu Josephat Lebulu katika makazi yake  rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti ambako pia alikutana na Maaskofu wa Makanisa
mbalimbali.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakitoa mkono wa  pole kwa watawa wa kanisa hilo wakati walipomtembelea Askofu Mkuu wa  Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Askofu Josephat  Lebulu katika makazi yake rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi  katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti ambako pia alikutana na Maaskofu wa Makanisa mbalimbali. Picha na IKULU

  • Share:

You Might Also Like

0 comments