MAJAMBAZI WA TATU WAPATA KICHAPO CHA MBWA MWIZI...

By Gadiola Emanuel - 10:08:00 AM

kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha Akili Mpwapwa akionyesha silaha ambazo majambazi hao walikutwa nazo

WATU watatu ambao ni majambazi wameuawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kuwapora wafanyabaishara watano waliokuwa wakielekea kwenye mnada wa soko la ng'ombe uliopo Meserani wilayani Monduli.

Majambazi hao wakiwa na silaha za moto, walikuwa wakitumia gari lenye namba T785 ACM aina ya Toyota Mark II ,walifyetua risasi nne hewani baada ya kuwavamia wafanyabiashara hao eneo hilo la Meserani na kuwapora kiasi cha sh. milioni 4.2 na simu mbili za mkononi.

Majambazi hao wametambulika kuwa ni,Obeid Erasto(30),Florence Basili(27) na Rafael Patrick(37) wote wakazi wa mjini Arusha.

Wafanyabishara hao wametajwa kwa majina kuwa ni, Jackson Kisyokii (47) Kijenge, Lembris Bikoto(60) Kisongo, Jackson Kalaine (35) ,Gregory Joseph (39) Kijenge na Silas Sayolo(40) Sokon 1ambao kwa pamoja walikuwa wakielekea kununua ng'ombe katika eneo hilo la Meserani wakitumia gari nambaT 744 BMX aina ya Hyundai.

Akizungumza na waandishi wa habari , Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa alisema tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 7 mchana katika eneo la Kisongo barabara ya Arusha- Babati ambapo majambazi hao waliwateka wafanyabiashara hao na kuanza kufyetua risasi hewani .

Mpwapwa alisema kuwa,wafanyabiashara hao walitii amri na kuwakabidhi majambazi hao kitita hicho na sumu za mkononi,hata hivyo baada ya kufanikiwa kupora waliamua kurudi mjini Arusha.

Walipofika eneo la Olmatejoo walihisi kufuatiliwa kwa nyuma na polisi ndipo walipolitelekeza gari walilokuwa wakilitumia na kuanza kukimbia kwa miguu .

Alisema kabla hawajafika mbali wananchi waliwazingira na kuanza kuwashambuliwa kwa mawe kiasi cha kupoteza fahamu ndipo polisi walipofika eneo la tukio .

Kwa mujibu wa kamanda Mpwapwa ,polisi kabla hawajawachukua majambazi hao walipekuliwa na kukuta wakiwa na bastola aina ya Brown ikiwa na risasi tatu yenye namba 069082 ,Bunduki aina Shortgun yenye namba R 253578 ikiwa na risasi 14 zikiwa zimefishwa kwenye gari walilokuwa wamelitelekeza.

Aidha pia,walikutwa na silaha iliyotengezwa kienyeji yenye namba 458 ikiwa na risasi tatu ,baada ya upekuzi huo polisi waliwachukua kwa ajili ya kuwafikisha hospitali ya Mount Meru wakiwa mahutihuti .

Aidha majambazi hao walifariki dunia muda mfupi wakiwa njiani kabla ya kufikishwa katika hospitali hiyo na uchunguzi juu ya tukio hilo bado unaendelea na kwamba polisi hawakufanikiwa kuokoa fedha zilizoporwa na majambazi hao.

  • Share:

You Might Also Like

0 comments