KAGAME CUP KUANZA JUNI 25 ,2011
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limekubali kuwa mwenyeji wa mashindano ya Kombe la Kagame yanayoshirikisha klabu bingwa za nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Klabu 12 zitashiriki katika mashindano hayo yatakayofanyika nchini kuanzia Juni 25 hadi Julai 9 mwaka huu. Tumechukua uamuzi huu mgumu wa kuandaa mashindano haya kwa lengo la kuyaokoa.
Awali mashindano hayo ambayo yalianzia nchini mwaka 1974 yalikuwa yafanyike Zanzibar ambayo ilijitoa. Baadaye yalihamishiwa Sudan ambapo napo yalikwama baada ya Serikali ya nchi hiyo kutokuwa tayari kuwa mwenyeji kwa sasa kutokana na sababu mbalimbali. Hivyo tunaziomba kampuni mbalimbali nchini zijitokeze kwa ajili ya udhamini ambao utawezesha kufanyika kwa ufanisi.
Jumatatu (Juni 20 mwaka huu) tutakuwa na mkutano na waandishi wa habari kuelezea taratibu za mashindano hayo ikiwemo timu zitakazoshiriki. Tanzania kwa kuwa mwenyeji itaingiza timu mbili.
0 comments