FREEMAN MBOWE YUKO HURU...

By Gadiola Emanuel - 2:07:00 PM

Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe, ameachiwa huru kwa dhamana na mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha mara baada ya kuonekana kuwa hakuwa na kosa lolote la kujibu mahakamani hapo.

Pia mdhamini wa awali wa mwenyekiti huyo Julius Margwe amekataliwa na mahakama hiyo kwa kushidwa kutii Mahakama na kumtaka mthamini mungine ambaye angeweza kufuata sheria za mahakama bila kuzikiuka.

Mahakama hiyo ya hakimu mkazi Arusha iliweza kumkubalil mthamini mungine ambaye alijitokeza kulichukua gurudumu hilo la mshitakiwa huyo,ambapo John Bayo ambaye ni Diwani wa kata ya Elerai wa CHADEMA ndie aliyekabidhiwa gurudumu hilo la kuwa mdhamini mpya wa Freeman Mbowe.

Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Charles Magesa akizungumza Mahakamani hapo, alisema kuwa kutokana na mdhamini huyo kukiuka masharti ya kuhudhuria mahakamani hapo, kwa sababu za kuwa na yeye anakabiliwa na kesi Mahakama ya Mwanzo Maromboso, hivyo mahakama imeamua kutoa nafasi kwa mdhamini mwingine.

Alisema kuwa mahakama imeona kuwa mdhamini huyu ana makosa na hata hawezi kueleza,Alisema kuwa mbali na kueleza uongo Mahakamani hapo kuwa alikuwa akifika mahakamani hapo, bado mahakama haina sababu naye sababu tayari ana kesi ya jinai ambayo hatma yake haifahamiki.

Kwa upande wa mshitakiwa ambaye ni mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe; Hakimu alisema ni kweli mahakama iliruhusu washitakiwa wabunge wahudhurie kikao cha bunge la bajeti na hivyo hawana sababu na Mbowe, ila kutokana na kukosekana kwa mdhamini wake, ndiyo sababu walitoa amri ya kukamatwa kwake.

Aidha magesa alibainisha kuwa mahakama hiyo inaendelea kuwapa ruhusa washitakiwa wote ambao niwabunge kutohudhuria mahakamani hapo hadi pale ambapo kikoa cha bunge kitamalizika ila aliwasisitiza wathamini wa washitakiwa hao kuhudhuria mahakamani hapa kila siku ambapo tarehe ya kesi imepangwa

Kabla ya Hakimu huyo kutoa maamuzi hayo, Hakimu huyo alimpa nafasi mdhamini wa Mbowe Julius Margwe na kumtaka aeleze sababu za kutofika mahakamani.

Akijibu maswali ya mahakamani hapo, Julius aliiambia Mahakama kuwa Mei 27 mwaka huu, hakufika sababu alikuwa na kesi Mahakama ya Mwanzo Maromboso na Mei 30 alifika mahakamani ila kwa sababu mahakama haikumpa nafasi kusema lolote hakujitokeza.

Naye Wakili upande wa Utetezi, Method Kimomogoro, aliiomba Mahakama hiyo, kuondoa amri ya kukamatwa kwa Mbowe na kutaka apewe dhamana yake ya awali, ili aweze kuhudhuria vikao vya bunge la bajeti ambalo yeye ni kiongozi wa kambi ya Upinzani.

Aidha Wakili huyo alimtetea mdhamini w ambowe kwa kutofika mahakamani na kusema kuwa hiyo ipo kwa kila mtu na hata wao kama mawakili wanasahahu tarehe za mahakama na ndiyo sababu huwa wanaandika, hivyo kw amwananchi wa kawaida ni lazima wasahahu tarehee.

Pia alipinga kauli ya wakili wa serikali ya kutaka mahakama impe onyo Mbowe kwa sababu kosa siyo lake na Mahakama ilimpa udhuru Aprili 29 mwaka huu, kesi hiyo ilipotajw ana kutoa sababu ya kuwa watakuwa katika vikao vya bunge la Bajeti na kuomba mahakama imrejeshee dhamana yake ya awali.

Upande wa Wakili wa serikali Juma Ramadhani, aliiomba mahakama hiyo itoe onyo kali kwa mshitakiwa kw akutofika mahakamani hapo na pia kumtaka mshitakiwa huyo na wenzake wawe na mawasiliano ya karibu na wadhamini wao, ili wasikose mahakamani hapo.


Alisema kuwa kuhusu dhamana ya Mbowe hana mashaka nayo, isipokuwa mdhamini wake hana uhakika na hajuwi nini anafanaya, hivyo hafai kuw amdhamini na kuomba mahakama kutoa uamuzi wa mdhamini huyo.

Baada ya pande hizo zote kuongea Hakimu alimwachia huru kw adhamana Freeman Mbowe na kutoa idhini ya kuendelea na bunge la bajeti hadi hapo Juni 24 mwaka huu, kesi hiyo itakapotajw atena.

Baada ya Freeman Mbowe, kuhachiwa huru na mahakamani hapo alipata nafasi ya kuzungumza na wafuasi waliofurika mahakamani hapo na waandishi wa habari, kwenye viwanja vya mahakama hiyo ambapo alisemaanapendakuwashukuru sana wananchi na viongozi wa chadema jinsi walivyojitokeza kumpa ushirikiano na kusema kuwa hiyo ni moja wapo ya kuwaonyesha serekalil nini maana ya nguvu ya uma.


Alisema kuwa anasikitishwa sana na kitendo ambacho serekaliwamekufanya cha kutumia nguvu kubwa kumlinda yeye na kusafirisha usiku wa huku akiwa chini ya ulinzi mkubwa kama kwamba yeye alikuwa nigaidi ambaye alikuwa na silaha .

“mimi nilijipeleka mwenyewe polisi sasa kama kweli ningekuwa na kimbia ningejipeleka sasa wao hawajaona hayo yote haitoshi wameamua kutumia nguvu kubwa sana maana wakati wakinipeleka uwanja wa ndege walikuwa na polisi wengi sana zaidi ya 50 yaani utathani ni gaidi anapelekwa alafu ndege ya kubeba watu mia ndo wameniweka mimi uko wakati hayo mafuta wangeyaweka ata kwenye kutengeneza vitanda vya hospitali wanatumia vibaya kodi za wananchi “alisema Mbowe.

Alisema kuwa serikali ilitumia ndege ya jeshi, ambayo ina uwezo wa kubeba watu 100, ambayo ilichukua watu watatu yaani yeye, Kamishina wa Polisi kanda kanda ya Ilala na Kamishna wa Polisi wa kikosi cha kuzuia ghasia wa Tanzania hadi KIA usiku wa majira ya saa 9.00.

Pia alisema mbali na kusafirishw akwa ndege hiyo kubwa, pia kulikuwa na magari nane ya FFU ambao walikuwa na mabomu na silaha kama wanasindikiza mwalifu.

Mbowe alisema kuwa kimsingi yeye hakuw ana kosa la kukamatwa na ndiyo sababu mahakama haikumuhoji hata swali moja kwa sababu waliona mwenye shida na mdhamini wake.


Alisema hakukuwa na sababu za msingi za kutumia rasilimali za serikali ambayo ni mali za umma na kumsindikiza kama muhalifu mtu ambaye hakuwa na hata na silaha.


Alisema kwamba anachoshukuru ni Polisi kutomfanyia unyama wowote na walikaa naye vizuri, isipokuwa alinyimwa haki yake ya msingi ya kuwa na uhuru wa kuwasiliana na watu.

Pia mara baada ya kesi hiyo kumalizika wananchi walimbeba kiongozi waho kwa juu huku wakiimba nyimbo za furaha.

Katika kesi hiyo ilihudhuriwa na wabunge 13 wa CHADEMA ambao ni Zito Kabwe, Halima Mdee, GodBleess Lema, Suzan Kiwanga,Ezekia Wenje, Christina Lisu,Paulina Gekulu,Israel Natse, Suzana Lyimo, Joseph Mbilinyi, Rahya Ibrahimu, ambaye ni Mbunge toka Pemba, Joyce Mukya na Joseph Selasini.

Wakati hayo yakiendelea mara baada ya kuaciw ahuru mshitakiw ahuyo, kulilipuka kelele za shangwe, huku wakiimba nyimbo za kumkataa Meya wa Manispaa ya Arusha, Gaudence Lyimo.

  • Share:

You Might Also Like

0 comments