JAMBAZI APATA KICHAPO CHA MBWA MWIZI MJINI A-CITY!!!

By Gadiola Emanuel - 10:16:00 AM

Mtu mmoja anaesadikiwa kuwa ni jambazi aliyetambulika kwa jina la Roberty Maji(35), mkazi wa Mbuguni amefariki dunia mara baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira kali katika eneo la standi ya mabasi madogo ya sanawari mjini hapa.

Akithibitisha kuuwawa kwa jambazi hilo, kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha Thobias Andengenye alisema kuwa tukio hilo lilitokea May 28 mwaka huu majira ya saa sita mchana ambapo mtuhumiwa huyo alikuwa akijaribu kuwakimbia wananchi kwa kutumia pikipiki yenye namba za usajili T224 AAW mara baada ya kufanya uhalifu katika eneo hilo

Alisema kuwa mtuhumiwa huyo mara baada ya kufanya uhalifu alikuwa akijaribu kuwatoroka wananchi wenye hasira kali ndipo wananchi hao walipoamua kuchukuwa mawe na marungu na kuanza kumpiga kila sehemu ya mwili wake hadi kumsababishia jambazi huyo kuanguka chini na kupoteza fahamu.

“sisi tulipata taarifa kuwa kunajambazi ambaye anapigwa katika maeneo hayo ya standi ya mabasi ya sanawari sasa polisi kwenda pale wakakuta jambazi huyu anapigwa na wananchi na tayari walikuwa wameshamvalisha tairi ndipo apo askari wakamsaidia na kumkimbiza hospitali lakini wakati akipelekwa akafia njiani”alisema Andengenye.

Alibainisha kuwa kwa taarifa za nyuma ambazo polisi wanazo zilikuwa zikionyesha kuwa jambazi huyo awali alikuwa akitafutwa na polisi kutokana na kosa la unyanganyi kwa kutumia silaha akiwa na wenzake pamoja na kosa la mauaji.

Andengenye alisema kuwa tukio la kwanza jambazi hilo lilifanya lilitokea May 21 ambapo mtuhumiwa huyo alidaiwa kuchukuwa tax yenye namba za usajili T 463 BNM katika eneo la metrople jijini hapa na kumuambia dereva taxi anaitaji kufika sanawari kuchukuwa wenzake na ndipo dereva huyo aliyetambulika kwa jina la Koentini Orema ambaye alifuata matakwa ya mteja wake na akaenda sanawari walipofika wakawachukuwa wenzake wanne na wakamwambia awapeleke kimandolu nje kidogo ya mji wa Arusha.

“wakati sasa anawapelekea ndipo walipotoa silaha na kumtishia na kumuamuru aachie gari ndipo alipoachia wakamteka na kumfunga na kamba kisha wakamtupa barabarani “alisema Andengenye.

Aidha alibainisha kuwa pia jambazi hili likiwa na wenzake linatuhumiwa kufanya uhalifu katika eneo la sokoine jijini hapa ambapo walimuuwa mlinzi aliyejulikana kwa jina la Josephy Kisunda wakati walipokuwa wakijaribu kuvamia mfanyabiashara wa mawe ajulikanae kama Sileshi Pandishi ambae anafanya biashara hiyo katika eneo hilo.

Andengenye alisema kuwa mwili wa marehemu umeifadhiwa katika hospotali ya mkoa ya maunti meru huku jeshi la polisi likiendelea ana upepelelezi wa kuwatafuta watuhumiwa wengine wa ujambazi walioshirikiana na marehemukufanya matukio hayo.

Alitoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi hata kwa kutoa taarifa pale tu ambapo wataona kunadalili za uhalifu au watakapo wanaona watu ambao wanawatilia mashaka.

  • Share:

You Might Also Like

0 comments