KOCHA WA MAN U , MOYES AWALALAMIKIA WAAMUZI HUKO ENGLAND

By Gadiola Emanuel - 4:17:00 AM

Meneja wa Manchester United, David Moyes amedai kuwa timu yake inacheza dhidi ya waamuzi pamoja na timu pinzani baada ya kushuhudia vijana wake wakipoteza mchezo dhidi ya Sunderland katika mechi ya nusu fainali ya kombe la Capital One.
Kocha huyo wa Manchester United alisikitishwa na uamuzi wa kuipatia Sunderland penalti na hivyo kuiwezesha kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
"Tunacheza dhidi yao(waamuzi) na timu pinzani kwa wakati mmoja," ameiambia Sky Sports.
"Kwa kweli inatisha. Tunaanza kuwacheka kutokana na maamuzi wanayotoa."
Mwaamuzi wa mchezo kati ya Manchester United na Sunderland, Andre Marriner aliwapa penalti wenyeji akishauriwa na mmoja wa wasaidizi wake baada ya Adam Johnson kuanguka katika eneo la hatari alipokabiliana na Tom Cleverley wa Manchester United.
Sunderland iliongoza kipindi cha kwanza cha mchezo kupitia kwa Ryan Giggs, aliyejifunga goli. Japokuwa Nemanja Vidic aliisawazishia timu yake mara baada ya kuanza kipindi cha pili, penalti iliyotolewa kwa vijana wa Borini, kunawapa Paka Weusi hao, "Black Cats" kuingia na ushindi katika mchezo wa marudiano utakaopigwa tarehe 22 Januari katika uwanja wa Old Trafford.
Katika kipindi cha wiki moja, Manchester United imeshuhudia kipigo kingine katika michezo ya kuwania vikombe huko England. Timu hiyo tayari imeng'olewa katika mashindano ya kuwania kombe la FA baada ya kucharazwa mabao 2-1 na Swansea.
Mapema mwezi huu Moyes alisema ilikuwa "kashfa" kwa Manchester United kunyimwa penalti dakika za mwisho katika mechi yao ya kuwania ubingwa wa ligi kuu ya England dhidi ya Tottenham. Katika mchezo huo uliofanyika uwanja wa Old Trafford, Manchester United ilitunguliwa mabao 2-0.
Hii ni mara ya kwanza kwa Manchester United tangu tarehe 22-26 Aprili 1992 kupoteza michezo mitatu ndani ya wiki moja. Source:BBC Sports

  • Share:

You Might Also Like

0 comments