MAKAMU WA RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA , DKT GHARIB BILAL AWATEMBELEA WAATHIRIKA WA MAFURIKO JIJINI DAR
By Gadiola Emanuel - 4:08:00 AM
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, akisalimiana na mmojawatoto waliohifadhiwa na wazazi wao
katika Kambi ya Shule ya Sekondari ya Azania, waliookolewa katika
maeneo yaliyojaa maji kutokana na mvua zilizonyesha jijini Dar es
Salaam kuanzia majuzi, wakati Makamu alipofika katika Kambi hiyo jana
Desemba 23, kwa ajili ya kuwapa pole waathirika hao.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akizungumza na Bi. Monica Luis, Mkazi wa Jangwani aliyeathirika
na mafuriko ya Mvua kubwa iliyonyesha jijini kuanzia majuzi, wakati
makamu alipotembelea katika Kambi ya Shule ya Sekondari Azania jijini
Dar es Salaam jana Desemba 23, kwa ajili ya kuwapa pole waathirika wa
mafuriko hayo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akizungumza na baadhi ya wananchi waliohifadhiwa katika Klabu ya
timu ya Yanga ya Jijini Dar es Salaam, wakati alipowatembelea kuwapa
pole wananchi hao walioathirika na mafuriko ya Mvua kubwa zilizonyesha
jijini kuanzia majuzi. Makamu alifanya ziara hiyo ya kutembelea baadhi
ya kambi za waathirika jana Desemba 23.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akisikiliza maelezo ya jinsi maji yalivyokuwa yamejaa wakati wa
mvua kubwa iliyosababisha mafuriko, kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Mecky Sadick (kulia), wakati alipotembelea kuwapa pole wananchi
waliokuwa wamehifhadhiwa katika Klabu ya Yanga, iliyopo Jangwani jana
Desemba 23.
Picha na Muhidin Sufiani-OMR
0 comments