RAIS JAKAYA KIKWETE AONGOZA MAMIA YA WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM KUUAGA MWILI WA ALIYEKUWA MTANGAZAJI WA TBC MAREHEMU HALIMA MCHUKA JANA.
By Gadiola Emanuel - 3:49:00 AM
Rais
Jakaya Kikwete akipeana mkono na Mkurugenzi Mkuu wa TBC Bw Clement
Mshana wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa mtangazaji Halim Mchuka leo
katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kabla ya kwwenda kuzikwa
makaburi ya Msasani baada ya Sala ya Ijumaa. | C.E.O wa blog ya wazalendo25 na gadiola25 I WISH YOU ALL THE BEST IN ALL PARTY AND HOLIDAYS.... I LOVE UUUU GUYZ ... |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, akisalimiana na mmojawatoto waliohifadhiwa na wazazi wao
katika Kambi ya Shule ya Sekondari ya Azania, waliookolewa katika
maeneo yaliyojaa maji kutokana na mvua zilizonyesha jijini Dar es
Salaam kuanzia majuzi, wakati Makamu alipofika katika Kambi hiyo jana
Desemba 23, kwa ajili ya kuwapa pole waathirika hao.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akizungumza na Bi. Monica Luis, Mkazi wa Jangwani aliyeathirika
na mafuriko ya Mvua kubwa iliyonyesha jijini kuanzia majuzi, wakati
makamu alipotembelea katika Kambi ya Shule ya Sekondari Azania jijini
Dar es Salaam jana Desemba 23, kwa ajili ya kuwapa pole waathirika wa
mafuriko hayo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akizungumza na baadhi ya wananchi waliohifadhiwa katika Klabu ya
timu ya Yanga ya Jijini Dar es Salaam, wakati alipowatembelea kuwapa
pole wananchi hao walioathirika na mafuriko ya Mvua kubwa zilizonyesha
jijini kuanzia majuzi. Makamu alifanya ziara hiyo ya kutembelea baadhi
ya kambi za waathirika jana Desemba 23.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akisikiliza maelezo ya jinsi maji yalivyokuwa yamejaa wakati wa
mvua kubwa iliyosababisha mafuriko, kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Mecky Sadick (kulia), wakati alipotembelea kuwapa pole wananchi
waliokuwa wamehifhadhiwa katika Klabu ya Yanga, iliyopo Jangwani jana
Desemba 23.
Rais
Jakaya Kikwete, akimwapisha, Dkt. Deodorus Kamala, kuwa Balozi wa
Ubelgiji, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha mabalozi wapya iliyofanyika
leo mchana Desemba 19, Ikulu Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete, akimwapisha, Phillip Marmo,
kuwa Balozi wa China, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha mabalozi
wapya iliyofanyika leo mchana Desemba 19, Ikulu Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete, akimwapisha, Dkt. Batilda Buriani, kuwa
Balozi wa Kenya, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha mabalozi wapya
iliyofanyika leo mchana Desemba 19, Ikulu Dar es Salaam.
Mabalozi wapya waliofia Ikulu Dar es Salaam leo kwa ajili ya kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete, wakisubiri kuapishwa.
Rais Jakaya Kikwete, akimwapisha, Ally A. Saleh, kuwa Balozi wa Oman,
wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha mabalozi wapya iliyofanyika leo
mchana Desemba 19, Ikulu Dar es Salaam.
Rais
Jakaya Kikwete, akimwapisha, Shamim Nyanduga, kuwa Balozi wa Msumbiji,
wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha mabalozi wapya iliyofanyika leo
mchana Desemba 19, Ikulu Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto), Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda (kuli) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Benard Membe, wakizungumza jambo, baada ya kumalizika kwa
hafla fupi ya kuwaapisha mabalozi wapya iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam
leo, Desemba 19.
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Benard Membe na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na Ushirikiano wa
Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, wakiwa katika picha ya pamoja na
Mabalozi wapya baada ya kuapishwa rasmi leo Ikulu Dar es Salaam. Picha
na Muhidin Sufiani-OMR
Shamim
Nyanduga, akipongezwa na Mumewe, baada ya kuapishwa rasmi kuwa Balozi
wa Msumbiji, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam leo.
Nyuma yao ni wanafamilia wa Familia hiyo.



