Mery
Kanyaga, akimpongeza binti yake, Shelder Boniface ambaye ni mshambuliaji wa
timu ya taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 20 ‘The Tanzanite’ muda mfupi
baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar
es Salaam , wakitokea Msumbiji katika mechi ya marudiano ya kufuzu fainali
za Dunia za wanawake ambako Tanzanite iliichapa Msumbiji mabao 5-1 huku Shelda
akitupia matatu kati ya hayo.
Mery
Kanyaga, akiwa amepozi na binti yake, Shelder Boniface mara baada ya
kuwasili akitokea Msumbiji na timu ya taifa ya wanawake ya Tanzanite.
Shelder aliifungia timu yake mabao matatu.
Nahodha wa The Tanzanite, Fatuma Issa akizungumza na waandishi wa habari.
Baadhi ya wazazi wakiwa na watoto wao baada ya kuwasili jijini Dar es Salam wakitokea Msumbiji.
Kocha Mkuu wa The Tanzanite, Rogasin Kaijage.
Baadhi ya wachezaji wa timu
ya taifa ya wanawake
chini ya umri wa miaka 20 ‘The Tanzanite’ wakipanda basi baada ya
kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
jijini Dar es Salaam, wakitokea Msumbiji.
Wachezaji
The Tanzanite wakiwapungia mikono mashabi waliofika kuwapokea kwenye Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana, wakitokea
Msumbiji.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura akipeana
mkono na wachezaji wa Tanzanite mara baada ya timu hiyo kuwasili jijini Dar es
Salaam ikitokea Msumbiji.
Wachezaji wa timu ya taifa ya wananwake chini ya
umri wa miaka 20 'Tanzanite' wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya
kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakitokea
Msumbiji katika mchezo wa kufuzu fainali za kombe la Dunia la wanawake dhidi ya
Msumbiji, ambako Tanzania ilishinda 5-1.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake
chini ya umri wa miaka 20 ‘The Tanzanite’ wakiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, wakitokea Msumbiji
katika mechi ya marudiano ya kufuzu fainali za Dunia za wanawake ambako
Tanzanite iliichapa Msumbiji mabao 5-1. Picha zote na Francis Dande
0 comments