AKIWA amesota mahabusu kwa takribani
siku 274 au miezi tisa hatimae
Msanii machachari wa filamu nchini Elizabeth Michael “Lulu”
anayekabiliwa na mashitaka ya mauaji bila kukusudia ya Steven Kanumba
ametoka mahabusu kwa dhamana.
Dhamana hiyo ilitolewa jana katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es
salaama baada ya kutimiza masharti ya dhamana yaliyotolewa jna Jaji Zainab
Mruke.
Alitimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili
wanaofanyakazi serikalini, ambao wamesaini hati ya Sh milioni 20 kila mmoja,
amewasilisha mahakamani hati zake za kusafiria, anatakiwa kuripoti mahakamani
tarehe mosi ya kila mwezi na kutosafiri nje ya Dar es salaam bila ruhusa ya
msajili wa mahakama.
Lulu alifikishwa mahakamani hapo jana saa 7:50 mchana akiwa
kwenye gari la polisi lenye namba za usajili STK 2823 na kufikishwa mbele ya
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam Francis Kabwe kwajili ya
kukamilisha taratibu za dhamana.
Mtuimishi wa Wizara ya Ardhi Florian
Mutafungwa pamoja na Dkt Verus Kataruga kutoka Wizara ya Afya ambapo saa 10:00 alitoka
chini ya ulinzi baada ya kukamilisha masharti ya dhamana.
Lulu
aliwasilisha maombi ya dhamana chini ya hati ya dharura akiomba
yasikilizwe na kuamriwa haraka kwa kuwa amekaa rumande kwa muda mrefu na
kosa lake lina dhamana.
Akitoa uamuzi wa ombi la dhamana ya Lulu
lililowasilishwa, Jaji Mruke alisema Mahakama imekubali ombi hilo kwa
kuwa, shitaka linalomkabili linadhaminika na dhamana ni haki yake ya
msingi .
Akizungumza baada ya kupewa dhamana, Lulu aliwashukuru watu wote walikuwa wanamsaidia katika kipindi chote tangu alipokamatwa hadi
anapata dhamana na kuomba
waendelee kumuombea.
“Nawashukuru watu wote lakini naomba muendelee kuniombea kwa
kuwa huu ni mwanzo tu kesi hii bado ndio kwanza inaanza” alisema Lulu huku
akitokwa na machozi.
Aliondoka na
gari gari lenye namba za usajili T 480 CFX Kwa upande wake Wakili wa Lulu, Peter Kibatala alisema,
dhamana ni mkataba kati ya mshitakiwa na mahakama na kuna taratibu za kufuata
ndio maaana walichelea lakini anashukuru msajili kwa kusubiri hata baada ya
muda wa kazi kuisha ili Lulu apate halki yake ya msingi.
Lulu alitakiwa kupewa dhamana juzi hata hivyo alirudishwa
rumande kwa kuwa alichelewa kuwasilisha mahakamani hati yake ya kusafkiria hadi
msajili alipoondoka baada ya saa za kazi kuisha.
Kesi hiyo ilifunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu huku Lulu akikabiliwa na mmashitaka ya kumuua Kanumba kwa kukusudia hata
hivyo baada ya upelelezi kukamilika, Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP)
alimbadilishia mashitaka na kuwa kuua bila kukusudia shitaka ambalo lina
dhamana.
Baadaye kesi hiyo ilihamishiwa katika Mahakama Kuu na
kusajiliwa kama shauri la kuua bila kukusudia lenye namba 125 ya mwaka jana, na
kupangwa kusikilizwa mbele ya Jaji Mruke. Hata hivyo kesi hiyo bado haijpangiwa
tarehe ya kuanza kusikilizwa.
Lulu anadaiwa Aprili 7 mwaka jana katika eneo la Sinza
Vatican, alimuua msanii Kanumba bila kukusudia.
Baada ya kutoka mahakamani Lulu alipokewa na Mama yake, na wasanii wenzake Dkt Cheni, Abdukarim Kenyata “Mc Kenyata na Muna pamoja na ndugu zake wengine. Na Father Kidevu Blog
0 comments