GIDABUDAY KATIKA HARAKATI ZA KUANZISHA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA

By Gadiola Emanuel - 9:19:00 PM

 Mwanariadha wa zamani na maarufu katika kuitanganza Tanzania katika masikio na macho ya mashabiki wa riadha duniani, maarufu kama WILHELM GIDABUDAY, wakati akizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha.

Gidabuday amesema kuwa lengo kuu la press conference hii ni kuwaomba watanzania kujitolea/kuonyesha uzalendo katika harakati alizozianzisha sasa za kuanzisha uchangiaji wa kuanzishwa kituo maalumu cha michezo cha Taifa. Namnukuu maneno haya "progress is a slow process", "huwezi kushinda vita kama huna eneo la kutrain wanajeshi wako" akimaanisha watanzania hatujachelewa kuanzisha kituo cha michezo cha taifa bali tunaweza kuanza sasa na tukafanikiwa, Pia maana ya pili ni hatutaweza kufanya vizuri katika michezo kimataifa bila ya kuwa na kituo maalum cha kufundishia wachezaji wetu.

Kuna maneno mengi mazuri na yakusikitisha  aliyozungumzia katika nyanja ya michezo katika AUDIO hio hapo chini. ISIKILIZE NA UCHUKUE HATUA LEO.

ISIKILIZE SAUTI HII YA MWANARIADHA MAARUFU "GIDABIDAY" MWANZO HADI MWISHO ALIYOZUNGUMZA NA VYOMBO MBALI MBALI VYA HABARI JIJINI ARUSHA.

 Mwandishi wa Channel 10  (kushoto mwanzo)akichukua tukio zima jijini Arusha.

Wadau wa Michezo nchini wakizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha;kutoka kushoto ni Gadiel Urio PR wa Shughuli hiyo, Rogath John Stephen(Mwanariadha wa kimataifa na Mtoto wa John Stephen Akhwari) , Bw. Wilhelm Gidabuday ambae ni mwanariadha na mwanaharakati wa Michezo Tanzania na Phaustin Baha Sule Mwana Riadha na Mshindi wa medali ya nusu marathon.
Katika kuonyesha moyo wa uzalendo  na nchi yeke bwana Gidabuday aliendelea kutoa wito kwa watanzania kuwa tayari kuchangia kuonyesha moyo wa kizalendo katika kuchangia kuanzishwa kwa kituo cha michezo cha Taifa. Wengine mwanzo kushoto ni Gadiola ambaye ndiye PR wa shuguri hii na katikati ni Rogath John Stephen(Mwanariadha wa kimataifa na Mtoto wa John Stephen Akhwari) 
Mwandishi mkongwe Adam Ihucha (kushoto) akiwa na mwandishi Gadiola Emanuel na PR wa harakati zote ulizoziona hapo juu wakiweka mambo sawa mudamfupi kabla ya press conference kuanza .

  • Share:

You Might Also Like

0 comments