AKIWA amesota mahabusu kwa takribani
siku 274 au miezi tisa hatimae
Msanii machachari wa filamu nchini Elizabeth Michael “Lulu”
anayekabiliwa na mashitaka ya mauaji bila kukusudia ya Steven Kanumba
ametoka mahabusu kwa dhamana.
Dhamana hiyo ilitolewa jana katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es
salaama baada ya kutimiza masharti ya dhamana yaliyotolewa jna Jaji Zainab
Mruke.
Alitimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili
wanaofanyakazi serikalini, ambao wamesaini hati ya Sh milioni 20 kila mmoja,
amewasilisha mahakamani hati zake za kusafiria, anatakiwa kuripoti mahakamani
tarehe mosi ya kila mwezi na kutosafiri nje ya Dar es salaam bila ruhusa ya
msajili wa mahakama.
Lulu alifikishwa mahakamani hapo jana saa 7:50 mchana akiwa
kwenye gari la polisi lenye namba za usajili STK 2823 na kufikishwa mbele ya
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam Francis Kabwe kwajili ya
kukamilisha taratibu za dhamana.
Mtuimishi wa Wizara ya Ardhi Florian
Mutafungwa pamoja na Dkt Verus Kataruga kutoka Wizara ya Afya ambapo saa 10:00 alitoka
chini ya ulinzi baada ya kukamilisha masharti ya dhamana.
Lulu
aliwasilisha maombi ya dhamana chini ya hati ya dharura akiomba
yasikilizwe na kuamriwa haraka kwa kuwa amekaa rumande kwa muda mrefu na
kosa lake lina dhamana.
Akitoa uamuzi wa ombi la dhamana ya Lulu
lililowasilishwa, Jaji Mruke alisema Mahakama imekubali ombi hilo kwa
kuwa, shitaka linalomkabili linadhaminika na dhamana ni haki yake ya
msingi .
Akizungumza baada ya kupewa dhamana, Lulu aliwashukuru watu wote walikuwa wanamsaidia katika kipindi chote tangu alipokamatwa hadi
anapata dhamana na kuomba
waendelee kumuombea.
“Nawashukuru watu wote lakini naomba muendelee kuniombea kwa
kuwa huu ni mwanzo tu kesi hii bado ndio kwanza inaanza” alisema Lulu huku
akitokwa na machozi.
Aliondoka na
gari gari lenye namba za usajili T 480 CFX Kwa upande wake Wakili wa Lulu, Peter Kibatala alisema,
dhamana ni mkataba kati ya mshitakiwa na mahakama na kuna taratibu za kufuata
ndio maaana walichelea lakini anashukuru msajili kwa kusubiri hata baada ya
muda wa kazi kuisha ili Lulu apate halki yake ya msingi.
Lulu alitakiwa kupewa dhamana juzi hata hivyo alirudishwa
rumande kwa kuwa alichelewa kuwasilisha mahakamani hati yake ya kusafkiria hadi
msajili alipoondoka baada ya saa za kazi kuisha.
Kesi hiyo ilifunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu huku Lulu akikabiliwa na mmashitaka ya kumuua Kanumba kwa kukusudia hata
hivyo baada ya upelelezi kukamilika, Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP)
alimbadilishia mashitaka na kuwa kuua bila kukusudia shitaka ambalo lina
dhamana.
Baadaye kesi hiyo ilihamishiwa katika Mahakama Kuu na
kusajiliwa kama shauri la kuua bila kukusudia lenye namba 125 ya mwaka jana, na
kupangwa kusikilizwa mbele ya Jaji Mruke. Hata hivyo kesi hiyo bado haijpangiwa
tarehe ya kuanza kusikilizwa.
Lulu anadaiwa Aprili 7 mwaka jana katika eneo la Sinza
Vatican, alimuua msanii Kanumba bila kukusudia.
Baada ya kutoka mahakamani Lulu alipokewa na Mama yake, na wasanii wenzake Dkt Cheni, Abdukarim Kenyata “Mc Kenyata na Muna pamoja na ndugu zake wengine. Na Father Kidevu Blog
GIDABUDAY KATIKA HARAKATI ZA KUANZISHA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA
By Gadiola Emanuel - 9:19:00 PM

Mwanariadha wa zamani na maarufu katika kuitanganza Tanzania katika
masikio na macho ya mashabiki wa riadha duniani, maarufu kama WILHELM GIDABUDAY, wakati akizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha.
Gidabuday amesema kuwa lengo kuu la press conference hii ni kuwaomba watanzania kujitolea/kuonyesha uzalendo katika harakati alizozianzisha sasa za kuanzisha uchangiaji wa kuanzishwa kituo maalumu cha michezo cha Taifa. Namnukuu maneno haya "progress is a slow process", "huwezi kushinda vita kama huna eneo la kutrain wanajeshi wako" akimaanisha watanzania hatujachelewa kuanzisha kituo cha michezo cha taifa bali tunaweza kuanza sasa na tukafanikiwa, Pia maana ya pili ni hatutaweza kufanya vizuri katika michezo kimataifa bila ya kuwa na kituo maalum cha kufundishia wachezaji wetu.
Kuna maneno mengi mazuri na yakusikitisha aliyozungumzia katika nyanja ya michezo katika AUDIO hio hapo chini. ISIKILIZE NA UCHUKUE HATUA LEO.
ISIKILIZE SAUTI HII YA MWANARIADHA MAARUFU "GIDABIDAY" MWANZO HADI MWISHO ALIYOZUNGUMZA NA VYOMBO MBALI MBALI VYA HABARI JIJINI ARUSHA.
Gidabuday amesema kuwa lengo kuu la press conference hii ni kuwaomba watanzania kujitolea/kuonyesha uzalendo katika harakati alizozianzisha sasa za kuanzisha uchangiaji wa kuanzishwa kituo maalumu cha michezo cha Taifa. Namnukuu maneno haya "progress is a slow process", "huwezi kushinda vita kama huna eneo la kutrain wanajeshi wako" akimaanisha watanzania hatujachelewa kuanzisha kituo cha michezo cha taifa bali tunaweza kuanza sasa na tukafanikiwa, Pia maana ya pili ni hatutaweza kufanya vizuri katika michezo kimataifa bila ya kuwa na kituo maalum cha kufundishia wachezaji wetu.
Kuna maneno mengi mazuri na yakusikitisha aliyozungumzia katika nyanja ya michezo katika AUDIO hio hapo chini. ISIKILIZE NA UCHUKUE HATUA LEO.
ISIKILIZE SAUTI HII YA MWANARIADHA MAARUFU "GIDABIDAY" MWANZO HADI MWISHO ALIYOZUNGUMZA NA VYOMBO MBALI MBALI VYA HABARI JIJINI ARUSHA.
Mwandishi wa Channel 10 (kushoto mwanzo)akichukua tukio zima jijini Arusha.
Moja vigezo vilivyoisukuma mahakama hiyo kumuachia uhuru ni kwa sababu shtaka lake linadhaminika, sharti la pili Lulu anatakiwa kusalimisha kwa msajili wa mahakama hiyo hati zake za kusafiria kutoka nje ya Jiji La Dar es Salaam bila idhini ya mahakama, na sharti la tatu, kuripoti kwa msajili wa mahakama kila mwezi.
Katika sharti la nne Lulu anatakiwa kuwa na wadhamini wawili kutoka serikali, na sharti la tano, wadhamini hao anapaswa kusaini bondi ya Sh20 milioni.
Awali jopo la mawakili wa Lulu ambalo linaongozwa na Wakili Kennedy Fungamtama, Makamu wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Petere Kibatala na Fulgence Masawe wa Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), wiki iliyopita waliwasilisha maombi ya dhamana kwa mahakama hiyo.
Maombi hayo, yalikuwa yamepangwa kusikilizwa wiki iliyopita na Jaji Zainabu Mruke, lakini yalipelekwa mbele mpaka yaani LEO Jumatatu siku ambayo amepewa dhamana.
Msanii huyo anakabiliwa na mashtaka ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa msanii maarufu wa fani hiyo nchini, Steven Kanumba.
Kesi hiyo ilifunguliwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu huku Lulu akikabiliwa na shtaka la mauaji ya kukusudia kinyume cha kifungu cha 196.
Katika hatua nyingine za kisheria baada ya upelelezi kukamilika, Desemba 21, mwaka jana, Mkurugenzi wa Mashtka (DPP) alimbadilishia Lulu Mashtaka na kuwa ya kuua bila kukusudia.








The 25 year old beat runners up Ada Ogunkeye (@Folustorms) and Kemi Owatemi (@SsmallzZ) to win the grand prize – a job contract with MTV Base worth 10 million Naira, and a brand new car!

Ukizungumzia mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya mwenye
sauti ya pekee (Personal Identity)
mwenye mashairi yaliokwenda shule na yanayogusa hisia na maisha ya kawaida ya kila siku hasa kwenye
maswala ya mapenzi …. Na inasemekana ni msanii anayeongoza kwa kupendwa na wanandoa
wengi hapa bongo kutokana na jinsi mashairi yake yanavyowagusa hasa wanandoa
ndani ya nyumba…..ni msanii pekee wa bongo fleva ambaye anawagusa sana watu
wazima kuliko msanii mwingine yeyote wa bongo fleva………. na si mwingine ni Linex ..!..... hivi punde tu
ametoka kuachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la MAHAKAMA YA MAPENZI………..
wimbo umetengenezwa Sweden kwa Fundi samweli sauti imerekodiwa na tuddy Thomas,
kwahiyo uandaaji mzima wa wimbo umefanywa na producer Fundi samweli (mzungu) ebu sikiliza wimbo huu jinsi fundi alivyopangilia muziki
huo kwa ustadi wa hali ya juu.
MSANII : LINEX
WIMBO : MAHAKAMA
YA MAPENZI
MTAYARISHAJI : FUNDI SAMWELI (FROM SWEDEN)
MTAYARISHAJI WA SAUTI : TUDDY THOMAS.
![]() |
| wit my NYC fam at #reincarnated screening @tonyyayo @50cent @officialbowwow @jordan_blue @adidas_originals |
![]() |
| me @busabuss @50cent @djtonytouch @therealdazdillinger #reincarnated |
Skylight Band yazidi kupasua anga za kimataifa katika muziki wa live Band jijini Dar es Salaam
By Gadiola Emanuel - 10:33:00 PM
Mmoja wa wapiga vyombo wa Skylight Band akionyesha kipaji chake cha kusakata sebene.
Ukawadia ule muda wa mduara na mambo yalikuwa kama hivi.....
Wema Sepetu na Zamaradi Mketema wakiserebuka.
Mdau akaomba kupata ukodak na warembo hao.
Mariam Nnauye na TID.
Mdau Benjamin katika pozi na mtoto wa ukweli.
Aneth Kushanba AK47
akiongoza safu ya vijana wa SKYLIGHT Band kutoa burudani kwa mashabiki
wake Ijumaa iliyopita kwenye kiota cha maraha Thai Village Masaki Jijini
Dar. Bendi hiyo inapiga hapo kila siku za Ijumaa kuanzia Saa 3 usiku.
Sura mpya ya SKYLIGHT Band
binti mrembo mwenye kipaji cha aina yake na sauti ya kumtoa nyoka
pangoni Salma Yusuf akitoa burudani kwenye ukumbi wa Thai Village Masaki
jijini Dar.
Mary Lukas akiimbia kwa hisia kali.
Kijana Sam Mapenzi (katikati), Aneth Kushaba AK47 na Joniko Flower wakiwa mzigoni.
Mzungu mmoja ambaye ni shabiki wa SKYLIGHT Band akimwaga mauno huko jasho likimtiririka samba samba na msanii Joniko Flower.
Watu weeeeee mzungu
noma......ilibidi watu waache kucheza na kumshangaa shabiki huyo wa
kizungu aliyekuwa kivutio kwa wengi hata mkongo haingii ndani kwa mauno
yake.
Pichani Juu na chini ni mashabiki wa Bendi hiyo wakijinafasi kwa raha zao.....Full kupagawa.....Chezea Skylight Band wewe...
Twende kazi..... Wera wera chapa ilale.......
Mwanamke nyonga hasa ukijaaliwa kuizungusha.
Mashabiki wa SKYLIGHT Band wakishow love.
Mwisho Mwampamba ndani ya nyumba.
Mdau Benjamin(katikati) akishow love na marafiki.
Mdau wa Michezo kutoka Clouds Fm Shaffi Dauda (wa pili kushoto) akishow love na marafiki.
Mashabiki wa SKYLIGHT Band wakila bata katika kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar es Salaam Ijumaa iliyopita.
Kila siku mashabiki wapya wanazidi kumiminika.....
Prof. Jay sambamba na mshikaji wake Kiboya nao walikuwepo.
Wadau wa SKYLIGHT BAND hawakukosa.








