Mzee Yusuf akiwadatisha mashabiki kwa ngoma zake kali.
Mzee Yusuf akicharaza gitaa.
Idris
Sultan akimtambulisha kwa mashabiki wa Dar Live mshikaji wake aliyekuwa
naye kwenye mjengo wa BBA, Samantha wa Afrika Kusini.
Mzee Yusuf akikandamiza kinanda wakati wa shoo yake Dar Live.
Mzee Yusuf na vijana wake wakifanya yao stejini.
Mzee Yusuf akionyesha ujuzi wa kucharaza gitaa chini kwa chini.
MFALME
wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' usiku wa Krismasi
amewadhihirishia mashabiki wake kuwa ni mfalme baada ya kufanya makamuzi
ya hatari katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem, jijini Dar kwenye
Tamasha la Wafalmelililodhaminiwa na VODACOM pamoja na COCACOLA.
Staa huyo aligonga ngoma zake zote na kuzikonga vilivyo nyoyo za mashabiki waliofurika katika uwanja huo wa burudani.
Mbali
na Diamond, Mfalme wa Taarab nchini, Mzee Yusuf naye alifanya shoo kali
na kuwapagawisha mashabiki waliofika kwa wingi kuliko siku zote katika
ukumbi huo wa kisasa wa Dar Live.
(PICHA ZOTE NA MUSA MATEJA / GPL)
0 comments