MKALI WA HIP HOP TANZANIA FID Q KATIKA TAMASHA LA FIESTA TABORA

By Gadiola Emanuel - 6:53:00 AM

Mkali wa Bongo Hip Hop Farid Kubanda a.k.a Fid Q akikamua vilivyo juu ya jukwaa na la Fiesta
Palikuwa hapatoshi usiku wa kuamkia leo ndani ya uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mjini Tabora,ambapo tamasha la Fiesta lilirindima.
Niki wa Pili kutoka kundi la Weusi akiwaimbisha mashabiki wake. 
 Shigiiiiidi shhheeeedddaaah...! Mtangazaji wa Clouds Fm,Adam Mchomvu akiwaimbisha wakazi wa mji wa Tabora na vitongoji vyake usiku wa kumkia leo katika tamasha la Fiesta lililofanyika ndani ya uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mjini Tabora
 Msanii anaefanya vyema katika anga ya muziki wa Bongofleva,Ommy Dimpoz akiwaimbisha mashabiki wake wimbo wa Nani kama mama.
 Kutoka THT,anaitwa Rachael akiimba jukwaani huku densa wake akinogesha mashabiki kimtindo.
Wasanii wa muziki wa hip hop ambao wanafanya vyema kwa sasa,Young Killer na Stamina kwa pamoja wakionesha umahiri wao wa kufoka foka mbele ya maelfu ya mashabiki wao (hawapo pichani),katika tamasha la Fiesta lililofanyika usiku wa kuamkia leo ndani ya uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mjini Tabora
Maelfu ya wakazi wa mji wa Tabora waliojotokeza kulishuhudia tamasha la Fiesta lililofanyika usiku wa kuamkia leo ndani ya uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mjini Tabora
Mkali wa mangoma kutoka Clouds FM,Dj Zero akikamua mangoma vilivyo.
Maelfu ya wakazi wa mji wa Tabora wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika tamasha la Fiesta lililofanyika usiku ndani ya uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mjini Tabora

  • Share:

You Might Also Like

0 comments