GIDABUDAY AMPONGEZA FILBERT BAYI NA SHULE YAKE

By Gadiola Emanuel - 6:26:00 AM




Filbert Bayi
Wiki chache zimepita tangu Chama Cha Riadha Tanzania (RT) kilipohitimisha mashindano ya riadha Taifa yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Pamoja na changamoto lukuki zinazokikabili chama hicho na viongozi wake wazoefu na wapya katika mikoa mbalimbali hapa nchini imeonyesa uwezo wa kuridhisha katika mchezo huo pekee uliowahi kuing'arisha taifa katika viwanya vikubwa duniani, Mkoa wa Pwani na Kagera ni miongoni mwa mikoa iliyojitahidi sana.
WANARIADHA CHIPUKIZI: Filbert Bayi, mwanariadha nyota wa zamani (The most Decorated Athlete in Tanzania) anastahili pongezi kwa kuwadhamini wachezaji chipukizi ambao ni taifa la kesho kimichezo. Wanariadha hao waliovutia washabiki wa riadha Mkoani Morogoro ni Tumaini Elisha, Joyce Moses, Nuruana Selestine, Rose Seif, Dorcus Boneface, Bitrina Michael, Agness Ernest, Regina Deo, Evodia Gabriel na Rehema Martin. 
Wanariadha hao chipukizi walizoa medali mbali mbali katika michezo ya Kuruka chini (Long Jump), Miruko mitatu (Triple Jump), Mita 200, Meta 400, Meta 800, Meta 1,500 na Kupokezana vijiti (Relay) ya 4/100, 4/400.


MAFANIKIO ZAIDI: Ni mwezi mzuri kwa Shule ya Filbert Bayi baada ya timu yake ya mchezo wa Pete (Netball) kutetea ubingwa wake mkoani Mbeya muda mfupi baada ya timu ya riadha ya  wanawake kuwezesha mkoa wa Pwani kushinda riadha taifa kwa upande wa wanawake.
Kwa hili la Netball bila shaka juhudi kubwa zilifanywa na mama Bayi (Anna Bayi) ambaye historia inathibitisha kwamba alikuwa balozi mzuri sana wa mchezo huo wa Pete. Kumekuwa na changamoto kubwa kipindi chote cha muendelezo wa Netball Tanzania bilashaka Bayi na mama Bayi wameteleza hapa na pale lakini lengo lao kubwa ni kuinua michezo nchini. La muhimu zaidi ni kwamba wameonyesha uvumilivu mkubwa (strength) hata pale wanapokosolewa hadharani pale inapobidi.

JUHUDI BINAFSI: Kinachofurahisha zaidi ni kwa jinsi gani wanafunzi hao walivyofanikiwa kupata mafanikio ya kuridhisha kwa muda mfupi tangu waanze kushiriki mchezo wa riadha. Bila shaka pongezi zinawahusu Filbert Bayi, kocha wa wanafunzi hao (Zackariah Gwandu) na wanafunzi wenyewe ambao "nidhamu na bidii zao zimewapa mafanikio" alisema mwanaharakati wa michezo nchini Wilhelm Gidabuday.

CHANGAMOTO: Binadamu anapobadili maisha kijiografia, kimasomo, kimichezo na hali ya hewa hupata mabadiliko ya kiafya lakini kisaikolojia pia. Hapo ndipo mahali ambapo ‘taaluma’ inachukua nafasi yake. Sina shaka kuamini kwamba juhudi za kitaluma zimechangia sehemu kubwa ya kuwawezesha wanafunzi hao kufanikiwa kimasomo na kimichezo kutokana na uzoefu mkubwa wa mafunzo wanayopata shuleni hapo.
Mheshimiwa Filbert Bayi aliwahi kunukuliwa akisema “Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni". Pamoja na tofauti zilizokuwepo kati ya viongozi wa chama cha riadha na mwanaharakati wa michezo nchini, "Mh. Bayi mimi leo ninasema, pongezi zinakuhusu kwasababu mazuri uliyoyafanya yalionekana Morogoro" alinukuliwa akisema mwanaharakati wa michezo nchini Gidabuday.

SOURCE: ASILI YETU TANZANIA

  • Share:

You Might Also Like

0 comments