Mshindi
wa shindano la Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS),Walter Chilambo
(Dar) akikabidhiwa sanduku lake lenye kitita cha shilingi milioni 50 ,ndani ya ukumbi wa Diamond jubilee,katika shindano hilo
lililovuta hisia za wengi,mshindi wa pili ameibuka mwanadada Salma
Abushiri (Zanzibar) na wa tatu ni Wababa Mtuka (Dar).
Mshindi
wa shindano la Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS),Walter Chilambo
(Dar) akiwashukuru wapenzi na mashabiki wake waliompigia kura na
hatimaye kuibuka mshindi wa shindano hilo,lililofanyika ndani ya ukumbi
wa Diamond jubilee.
Baadhi
ya mashabiki wa mshindi wa shindano hilo la EBSS,Walter Chilambo
wakishangilia kwa shangwe na vifijo mara baada kutamkwa yeye ndiye
kinara katika kilele cha shindano hilo lililovuta hisia za watu wengi.
Mkurugenzi
wa kampuni ya Benchmark Productions Limited, na jaji mkuu wa Shindano
la Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS) Mada Rita, akiwa amemkumbatia mshindi wa
shindano hilo Walter Chilambo ndani ya ukumbi wa
Diamond,Chilambo ameibuka na kitita cha shilingi Milioni 50 za Kitanzania.
Msanii Barnaba akiimba na mmoja wa washiriki wa shindano la Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS).
0 comments