DJ WA NIGERIA KUFANYA ONYESHO NA KUTOA MSAADA KWAJAMII JIJINI DAR ES SALAAM
By Gadiola Emanuel - 2:10:00 PM
Mtengenezaji wa muziki, mtunzi wa nyimbo na DJ raia wa Nigeria anayefanya kazi zake nchini Marekani Bi.Florence Ifeoluwa maarufu kama DJ Cuppy akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Slipway jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wa habari wakiwa na Dj Mtengenezaji wa muziki, mtunzi wa nyimbo na DJ raia Nigeria katika hoteli ya Silpway jijini Dar es salaam.
DJ Cuppy.
MTENGENEZAJI wa muziki, mtunzi wa nyimbo na DJ raia wa Nigeria anayefanya kazi zake nchini Marekani Bi.Florence Ifeoluwa
maarufu
kama DJ Cuppy amewasili jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara
yake ya Afrika yenye jina la 'Cuppytakes Africa'.
Wakati
akiwa jijini hapa Dj huyu ambaye ni maarufu sana alitembelea kituo
chaKigamboni Community Center kinachotoa elimu kwa watoto wanaoishi
katika mazingira magumu.
Ziara
yake ilihitimishwa na onyesho la muziki lililofanyika katika hoteli ya
Slipway,tarehe 16 Agosti,Ziara yake hii kabambe ya mwezi mzima ilianza
Agosti 1 jijini Lagos, Nigeria ikifuatiwa naSenegal, Ghana na Kenya.
Tanzania
ni nchi ya tano katika ziara yake na hapo DJ Cuppy atatembelea nchi za
Rwanda, Uganda na Afrika Kusini.“Nilikuwa na ndoto ya kutembelea Afrika,
lengo kuu likiwa ni kujionea utamaduni wake, ndotohii sasa imetimia,"
alielezea katika mkutano na waandishi wa habari mjini Lagos Julai 8
hukuakiongeza kwamba “nina furaha sana kuonja radha ya muziki tofauti na
kupata uzoefu kutokanana ziara hii!" Alisema.
Pamoja na
hayo, ziara hii inalenga kutoa msukumo katika jamii kwa kila nchi,
DJ huyu mwenyekusherehesha ana shauku juu ya elimu ya viongozi wa
baadaye wa Afrika.
Kupitia
msaadamkubwa wa asasi ya Dangote Foundation, anatembelea na kutoa
msaada kwa shirika lisilo lakiserikali katika kila nchi
atakayoitembelea.
Hapa
Cuppy ametembelea kituo cha jamii cha Kigamboni kijulikanacho kama
(KCC), Kituo hiki huwa kinashughulika na masuala ya kutokomeza umaskini,
huku kikijikita katika kutoa elimu ya chekechea na msingi kwa watoto
ambao wako mbali na upatikanaji waelimu.
KCC
pia hutoa fursa nyingine za kujifunza kwa vijana wa Kigamboni, na pia
hutoa elimu
ya jamii, madarasa ya kuendeleza vipaji na mafunzo ya ufundi stadi,
Ziara hii inayojulikana kwa jina la “Cuppy takes Africa” wamechagua
kituo hiki kwa sababu ya kujitolea kwao kukuza vipajina kujenga
upatikanaji wa elimu kwa jamii.
DJ
Cuppy amefanya kazi katika safu ya tuzo yenye hadhi ya juu ikiwa ni
pamoja na FinancialTimes Summit mwaka 2014 na kwenye tuzo za muziki za
MTV Afrika. Yeye ni msomi kutokaChuo cha London King’s College na sasa
anaendelea na masomo ya shahada ya uzamili katika
fani
ya Sanaa na biashara ya muziki kwenye Chuo Kikuu cha New York. Cuppy
pia ni balozi wautalii wa Nigeria.Ziara hii ya “Cuppy takes Africa”'
inayojumuisha maonyesho, mashirikishano ya wasanii, fursaza vyombo vya
habari na ushirikiano wa hisani umedhaminiwa na benki ya GT.
Kuhusu DJ Cuppy:
Cuppy
ni DJ, producer wa muziki na mtunzi wa nyimbo.alizaliwa jijini Lagos
mwaka 1992. Cuppy alianza kufanya uzalishaji wa muziki na baadayekuwa
mchezesha muziki (DJ) akiwa na umri wa miaka 17.Cuppy mara nyingi
amekuwa na bahati ya kuwa DJ kwenye umati wa watu wasomi wakimataifa;
alitoa burudani mbele ya wanadiplomasia kwenye mkutano wa Financial
Times Luxury mwaka 2014, ambao ulifanyika jijini Mexico City. Alikuwa
pia DJ katika jarida la Tatlerna Christie Inc Arts Ball, ambao
ulifanyika jijini London ikifuatiwa na matukio mengi yaushirika mjini
Dubai. Kuchaguliawa kwa Cuppy kuwa Dj wakati wa tuzo za muziki za MTV
Afrika mwaka 2014 mjini Durban, ilikuwa ni fahari kwa mashabiki wa Cuppy
duniani kote.
Mwaka
jana mwezi Julai 2014, Cuppy ilitoa tepu yake iliyokuwa na mafanikio
makubwailiyojulikana kwa jina la House Of Cuppy. Ikiwa na mkusanyiko wa
radha ya muziki tofauti wawasanii wa kinigeria waliokuwa
wanafanya vizuri kimuziki nchini Nigeria. House Of Cuppyilizinduliwa kwa
mafanikio jijini London, Lagos na New York.Cuppy aliteuliwa na
Mheshimiwa Waziri wa Utamaduni na Utalii tarehe 17 Aprili 2014
kuwa Balozi wa utalii nchini Nigeria. Kwa sasa yeye ni nembo ya
kuchochea kampeni ya kuitangaza Nigeria.
“Cuppy ni kijana mjasiriamali, na ni dhahiri anapaswa kuigwa.
0 comments