Ben Pol, Wangechi watisha ‘Coke Studio Afrika’ Kenya

By Gadiola Emanuel - 8:14:00 AM


 Msanii wa kizazi kipya na mkali wa miondoko ya R&B Ben Pol akitumbuiza katika jukwaa la Coke Studio wakati wa tamasha la Coke Studio Afrika msimu wa tatu lililofanyika mwishoni mwa wiki nchini Kenya. Wasanii wengine walikuwepo katika tamasha hilo ni Wangechi (Kenya) pamoja na Silver Stone (Ghana)
 Msanii wa kizazi kipya na mkali wa miondoko ya R&B Ben Pol kutoka nchini (kulia) na Wangechi kutoka Kenya wakitumbuiza katika jukwaa la Coke Studio wakati wa tamasha la Coke Studio Afrika msimu wa tatu lililofanyika mwishoni mwa wiki nchini Kenya.
 Msanii wa kizazi kipya na mkali wa miondoko ya R&B Ben Pol kutoka nchini (kushoto) na Wangechi kutoka Kenya wakitumbuiza katika jukwaa la Coke Studio wakati wa tamasha la Coke Studio Afrika msimu wa tatu lililofanyika mwishoni mwa wiki nchini Kenya.
 Msanii maarufu wa miondoko ya Hiphop kutoka nchini Kenya Wangechi akitumbuiza katika jukwaa la Coke Studio wakati wa tamasha la Coke Studio Afrika lililofanyika mwishoni mwa wiki nchini Kenya
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Wangechi (Kenya), Ben Pol (Tanzania) na Silva Stone (Ghana) walitumbuiza katika jukwaa la Coke Studio wakati wa tamasha la Coke Studio Afrika lilofanyika nchini Kenya mwishoni mwa wiki.

Na mwandishi wetu.
Msimu wa tatu Coke Studio Afrika  umeanza ambapo 
 ilishuhudiwa  wasanii Ben Paul kutoka Tanzania na Wangechi (Kenya) na Silver Stone (Ghana) wakitumbuiza katika jukwaa la Coke Studio na kuamsha nderemo na vifijo kwa mashabiki ambao walihudhuria tamasha hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki hii nchini Kenya.
Nyimbo iliyoonekana kukonga nyoyo za mashabiki  katika tamasha hilo ni ile ya ‘Sophia’ ambayo aliimba kwa kushirikiana na Wangechi, ambapo inataja moja kwa moja mji wa Dodoma, ambao ndio makao makuu ya hapa nchini.
Msimu huu wa Coke Studio umeambatana na kampeni mpya yenye jina la ‘Sababu Bilioni za Kuamini’, na hivyo kujumuisha vijana mbalimbali ambao wanaamini katika kufikia malengo yao bila ya kujali changamoto zinazowakabili.
Katika tamasha hilo kulikuwa na vijana watano kutoka Tanzania wenye vipaji mbalimbali ambao walipata fursa ya kujifunza kupitia mambo mbalimbali baada ya kueleza namna wanavyojiamini katika kutimiza ndoto zao.
Vijana hao ni Minaeli Benedict, Stanley Meshack Mafundo, Hassani Singizi, Jackson, Shabani Swaibu (wote kutoka Dar es Salaam) na Jackson Kassian (Morogoro).
Baada ya kumalizika kwa tamasha hilo, vijana hao walipata fursa ya kuzungumza na wasanii hao ambao pia ni vijana kabisa, na kuelezwa mbinu ambazo zitawawezesha kupambana na hatimaye kufikia ndoto zao.
Katika kuhakikisha vijana hao hawakati tamaa kufikia malengo yao, Ben Pol aliwaambia kwamba, mpaka kufikia mafanikio aliyonayo sasa, amepitia changamoto nyingi sana ikiwemo kunyimwa nafasi ya kurekodi nyimbo zake na waandaaji mbalimbali wakiamini kuwa hakuwa na uwezo wa kuimba lakini licha ya kufanyiwa hivyo aliendelea kupambana mpaka kufanikiwa kufika alipo sasa.
“Ninachotaka kuwaambia ni kwamba, mfano, kwa wale wenye vipaji vya kuimba, kitu kikubwa unachotakiwa kufanya ni kuwa na nyimbo nyingi ambazo, hata ukirekodi moja isipofanya vizuri, unatoa nyingine ili kuhakikisha unaendelea kusikia masikioni kwa watu”, alisema
“Kitu kingine ni kwamba unaposimama mbele ya watu,  waone ni wa kawaida tu na wala usiwagope, bila ya kujali nyadhifa zao isipokuwa kikubwa ni kutowaonesha dharau”, alisisitiza.
Wangechi kwa upande wake alisema : “ Vijana wa jinsia zote ni muhimu kujiamini na kuondokana na dhana kwamba jinsia fulani ndio wanaweza kitu fulani, kwa mfano mimi naweza kufanya ‘hiphop’ na R&B, sasa wasichana wengi hata kama wanaweza, huogopa kufanya Hiphop wakiamini kwamba ni mziki wa kiume lakini kumbe yeyote anaweza kuimba”.
Lengo kuu la Coke Studio Afrika ni kuwakutanisha kwa pamoja wasanii wenye mbalimbali wa Afrika na kuimba nyimbo ambazo zina vionjo tofauti hivyo kuongeza msisimuko. Lakini vilevile kutoa fursa kwa wasanii wachanga  kushirikiana na wakubwa ili kuwapa changamoto ya kuongeza ujuzi katika kazi zao na kuzidi kukuza vipaji vyao

Katika msimu huu wa Coke Studio Afrika, ni wasanii kutoka mataifa matano tu tu ndio wamechaguliwa  kutumbuiza. Mataifa hayo ni Nigeria, Msumbiji, Kenya, Uganda na Tanzania.

  • Share:

You Might Also Like

0 comments