MWANAMUZIKI JHIKOMAN AMESHATUA TUBINGEN, UJERUMANI ATATUMBUIZA NDANI YA 5th International African festival Tubingen 2014
By Gadiola Emanuel - 9:24:00 AM
Kutoka Bagamoyo ,Tanzania hadi Kimataifa ! Ujerumani Kutingishwa na Muziki!
Tübingen,Ujerumani
Mwanamuziki nyota wa reggae barani Afrika Jhiko Manyika
aka Jhikoman kutoka Bagamoyo,Tanzania amewasili mjini Tubingen,Ujerumani
kwa ajili ya kushiriki katika maonyesho makubwa ya 5th International
African Festival Tübingen 2014,yatakayo anza 17 julai 2014 mpaka 20 Julai 2014 katika viwanja ya Festplatz,mjini Tübingen. watayarishaji wa maonyesho hayo
Afrikaktiv.org wamemtaja mwanamuziki Jhikoman kuwa ni nyota inayong'aa kutoka Afrika na wamemwalika kwa ajii ya kuja kuzidisha mwangaza katika soko la ulaya. Mkurugenzi wa maonyesho hayo Madam Susan Tatah alisema kuwa ujio wa mwanamuziki Jhikoman nchini
Ujerumani unazidisha uhusiano mzuri katika sekta ya sanaa na utamaduni
kati ya Ujerumani na Tanzania pia Afrika kwa ujumla,Madam Susan Tatah
alisema ujio wa Jhikoman una maana kubwa kwa wajerumani kwa mwanamuziki
huyo anatoka katika mji wa Bagamoyo ambako ndipo palikuwa makao makuu ya
serekali ya ukoloni ya kijerumani na ndipo wajurumani walipojenga shule
ya mwanzo Afrika Mashariki, Madam Susan Tatah alisema Jhikoman pia
atatia sahini
mkataba wa ushirikiano wa kudumu wa "Cultural Exchange program" pamoja Afrikaktive pia na mji wa Tübingen.
0 comments