Tusker Project Fame 6 : Hope wa Burundi ashinda shindano la Tusker Project Fame 6

By Gadiola Emanuel - 3:13:00 AM

Hope wa Burundi ashinda shindano la Tusker Project Fame 6
Hope aliwabwaga waimbaji wa Kenya, Amos na Josh waliokuwa kipenzi cha wengi na ambao waliaminika wangeweza kuwa washindi.
Baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa shilingi milioni 5 za Kenya (takriban shilingi milioni 100 za Tanzania) Hope hakuamini masikio yake na alilala chini kwa furaha huku baadaye akionekana kutaka kuanguka kwa butwaa kubwa aliyokuwa nayo na washiriki kumshikilia.
Mshindi huyo wa Tusker Project Fame 6 amejishindia pia mkataba wa mwaka mmoja wa kurekodi chini ya record label ya Sony Music Africa.
Nafasi ya pili imekamatwa na Wakenya hao, Amos na Josh na kufuatiwa na Daisy wa Uganda huku mwakilishi wa Tanzania, Hisia akikamata nafasi ya nne.
Katika fainali hiyo, washiriki walioingia tano bora walitumbuiza nyimbo zao wenyewe walizozirekodi na pia kuoneshwa video za nyimbo hizo.

  • Share:

You Might Also Like

0 comments