M-PESA KWA SASA KUTUMIA ATM ZA DTB KUTOLEA FEDHA

By Gadiola Emanuel - 2:11:00 AM


    Mkuu wa Kitengo cha Uzalishaji na Masoko wa DTB, Sylvester Bahati,(kushoto)akiwaelezea waandishi wa habari,jinsi ya kutoa fedha  kwenye mashine za kutolea fedha za DTB kupitia huduma ya Vodacom M PESA ambapo sasa wateja wanaotumia huduma hiyo wanaweza kutoa pesa kupitia mashine hizo popote walipo nchini,huduma hiyo imezinduliwa leo jijini Dares Salaam pamoja nae ni Meneja mahusiano ya nje wa Vodacom Tanzania,Bw.Salum Mwalim.

      Meneja mahusiano ya nje wa Vodacom Tanzania,Bw.Salum Mwalim,akitoa fedha kwa mara ya kwanza baada ya kuzinduliwa kwa huduma ya kutoa fedha kupia mashine za kutoa fedha za DTB kupitia huduma ya M PESA, ambapo sasa wateja wanaotumia huduma hiyo wanaweza kutoa pesa kupitia mashine hizo popote zilipo nchini anaeshuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha Uzalishaji na Masoko wa DTB, Sylvester Bahati.

      Meneja mahusiano ya nje wa Vodacom Tanzania,Bw.Salum Mwalim,pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Uzalishaji na Masoko wa DTB, Sylvester Bahati.wakifurahia mara baada ya kutoa fedha kwa mara ya kwanza kupitia mashine za kutoa fedha za DTB kwa huduma ya M PESA, ambapo sasa wateja wanaotumia huduma hiyo wanaweza kutoa pesa kupitia mashine hizo popote zilipo nchini.

  • Share:

You Might Also Like

0 comments