AMBASSADORS OF CHRIST FROM KIGALI NDANI YA TAMASHA LA PASAKA
By Gadiola Emanuel - 9:04:00 AM
Na Mwandishi Wetu
IDADI ya wasanii wa nje
watakaokuja kutumbuiza kwenye Tamasha la Pasaka mwaka huu imezidi
kuongezeka na sasa Wanyarwanda nao wamethibitisha kushiriki.
Mwenyekiti wa Kamati ya
Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema jana kuwa kwaya ya
Ambassadors of Christ ya Kigali Rwanda inayotamba na albamu ya Mtegemee
Yesu imethibitisha kushiriki tamasha hilo litakalofanyika Machi 31 mwaka
huu jijini Dar es Salaam.
“Watakuja kung’arisha tamasha la
mwaka huu na wamejipanga vya kutosha kuhakikisha mashabiki wanapata
burudani ya nguvu, nia yetu ni kuwa na wasanii wakubwa Afrika na hilo
ndilo tutakalolifanya mwaka huu.
“Kabla ya Jumatano tutatangaza
msanii mkubwa mwingine ambaye bado tunaendelea na mazungumzo naye
kuhakikisha mambo yanakuwa safi, ili aje kutumbuiza kwenye tamasha
letu,” alisema Msama. Alieleza kuwa katika albamu yao
hiyo ina nyimbo nane ambazo ni JY’ Ushima Uwite, Mtegee Yesu, Ndifuza
Kugerayo, Iyana Iby’ Isi, Yesu Niwe Mungeri, Parapanda, Abasaruzi na
Nenda.
Wasanii wengine wa nje ya
Tanzania ambao tayari wamethibitisha kushiriki tamasha hili ni , Ephraim
Sekeleti wa Zambia na Solomon Mukubwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Congo (DRC) anayeishi Kenya. Wasanii wa Tanzania ni Rose Muhando,
Upendo Nkone na John Lissu.
Tamasha la Pasaka litafanyika Dar
es Salaam Machi 31 na litaendelea Aprili mosi kwenye Uwanja wa Sokoine
Mbeya, wakati Aprili 3 ni Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 Uwanja wa
Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba,
Mwanza.
0 comments