Nachukua fursa hii,kuwashukuru WanaIgunga(Ingawa wengi hawana uwezo wa
kuwa kwenye computer kama mimi na wewe)Nawashukuru wote waliotutia
moyo,nawashukuru hata wale ambao hawakututia moyo,Nawashukuru sana
Uchaguzi Igunga umeisha,mengi yamesemwa na kuandikwa kuhusu mchakato
mzima,kuna mengi sana yalitokea na mimi nimeyashuhudia.Kwanza nikiri
kuwa ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika Igunga,kimsingi nilitarijia
Igunga yenye neema,na maisha bora,lakini nilikumbana na UFUKARA wa
kutisha,na maeneo mengine hata Kiswahili hawajui kwani vijana wadogo
sana wa umri chini ya miaka 25 hawajaenda shule,amezaliwa hapo hapo
kijijini,amekulia hapo kijijini,na hajui maisha mengine zaidi ya maisha
ya shida hapo kijijini.Wanawake wanatembea hadi kilometa 15 kufuata maji
ambayo kimsingi si safi wala salama. Lakini katika lindi kubwa la
umaskini wa Igunga,bado serikali ya CCM imatumia mabilioni ya pesa
kurudisha jimbo la IGUNGA,ni wazi siasa za Igunga zilikuwa za nguvu
kupita kiasi,kwa mara ya kwanza katika historia ya Taifa letu
tumeshuhudia uvunjivu,mkubwa wa sheria na katiba.Mimi ni mmojawapo wa
waadhirika wakubwa wa siasa za visasi,na matumizi makubwa ya
nguvu,nilitekwa na vijana wa green guard,na kunitupa porini,baada ya
purukushani kubwa,nikaripoti polisi lakini hakuna hatua
zilizochukuliwa,na mwisho wakanigeuzia kibao et mimi ndio
niliwateka,(Aibu kwa jeshi letu la polisi,historia itawahukumu)
Nimeshuhudia dini ikiingilia siasa,na kuwataka waumini wao kutokichagua
chama fulani,huu ni moto uliopandikizwa kwa makusudi kabisa,yaani chama
tawala kimeishiwa hoja,hata kufikia mahali pa kuwatumia viongozi wa
DINI,ili tu kujihakikishia uhalali wa kubaki madarakani,na bila aibu
viongozi wetu wastaafu,na wazee wa heshima kwenye hili taifa wakakaa
kimya,hakuna hata mmoja aliyekemea tabia hii(Historia itahihukumu ccm
kwa kkupandikiza chuki ya dini kwenye taifa letu,aibu kubwa kwa ccm)
.Nimeshuhudia wanawake wakinyanyaswa na polisi eti tu ni wafuasi wa
CHADEMA,hakuna hata mmoja aliyekemea,DC aliyevunja sheria yeye kwa kuwa
tu ni DC na ni kada wa ccm,akaonekana amedhalilishwa.Nimeshuhudia vijana
wengi wakibambikiziwa kesi,kwa kuwa tu ni wafuasi wa
CHADEMA,ninapoandika sasa kuna vijana watano walishika gari ya
mwenyekiti wa ccm wilaya ya Igunga akigawa hela rushwa,wakaripoti
polisi,na baada ya polisi kukagua gari hiyo wakakuta begi lina zaidi ya
21milion,vijana wale wazalendo wakawekwa chini ya ulinzi,eti ni
wanyanganyi wanotumia silaha,na bila utu wala heshima kwa binadamu
wenzao,polisi wakawapelea Nzega siku ya Ijumaa,hadi Jumatatu
walipopelekwa mahakamani na kusomewa shitaka la unyanganyi wa kutumia
silaha,Vijana wale walisekwa ndani kwa siku tatu bila chakula wala
maji,,u wapi utu wa na usawa wa binadamu?tunaelekea wapi kama taifa?na
misingi gani ya taifa tunajenga? Uchaguzi wa Igunga umekuwa na mengi
ya kujifunza,kwa serikali ya ccm,wametumia rasilimali zetu,kwa ajili ya
Igunga tu,ni aibu kwa ccm na viongozi wake,lakini kubwa na ambalo
sharti wajifunze ni kuwa ,inapofika mahali Chama dola,chenye
serikali,rasilimali pesa,rasilimali watu,uongozi kuanzia balozi wa
nyumba kumi,kulalamikia CHAMA CHA UPINZANI,eti kinagawa hela,eti
kimeingiza makomandoo,na Mungiki,ni wazi kuwa CCM kimepoteza mwelekeo na
sasa kinaelekea kwenye anguko kuu. Kimsingi Dr Kafumu hajachaguliwa
na wanaIgunga,amewekwa na DOLA na DOLA hiyohiyo itamwondoa,ni swala la
muda,kwa ukiukwaji huu wa sheria,kanuni,utu wa binadamu,kamwe hatodumu
kwenye kiti cha DAMU,kwa zaidi ya mwaka. Ni faraja iliyoje kuona
kuwa sasa ukombozi wa pili wa taifa letu u karibu kuliko mategemeo ya
wengi,kuna wengine wataona ni maneno ya kujifariji baada ya kushindwa
Igunga.Lakini huu ndio ukweli na ccm ni mashahidi katika hili,wanajua
nguvu kubwa kiasi gani walitumia kulikomboa na kutunyanganya ushindi
Igunga,na bila msaada wa vyombo vya dola wasingeweza. Uchaguzi
umeisha,kuna majeruhi wengi,na ambao kesho ndio wapamabanaji wa
ukweli,Jambo moja la msingi ni kwamba hakuna wingi wa
silaha,risasi,mabomu,wala vifaa vya kisasa vya kijeshi vinavyoweza
kuzuia umma unaotaka mabadiliko,umma uliochoka,umma unaolilia
ukombozi,na kwa kadri serikali inavyozidi kuminya uhuru na demokrasia
ndivyo umma unavyozidi kuamka na kupigania uhuru wao.Daima tutasonga
mbele Aluta continua….. Na saa ya ukombozi ni sasa.............
Nanyaro Ephata Nanyaro diwani kata ya Levolosi,Arusha-BAVICHA
0 comments