UNAMFAHAMU MTU ANAITWA 'MTAKASAJI?'

By Gadiola Emanuel - 11:52:00 PM

Jamani leo asubuhi nilikuwa nasikiliza kipindi kimoja cha Radio moja maarufu hapa Tanzania ,katika kipindi chake kinachoita PB saturday.
Nilishtushwa sana na hilo neno la Mtakasaji;huyu ni nani?fuatilia unipe maoni yako na ushauri nini cha kufanya.

Huko Mkoani Mara ,Ukerewe kuna watu wanajiita watakasaji,hawa watu ni Wanaume ambao mke anapofiwa na mumewe wao hufanya nao Tendo la Ndoa wakidai kuwa wanawatakasa,kwa fikra kuwa huyu mama huwa ni mchafu na ni mweusi ,kwa hiyo anatakiwa kusafishwa kwa kutakaswa .Wanaume hawa ni wale ambao hawajawahi kuoa na wanafanya kazi hiyo ya kutakasa.....aliekuwa anasimulizia kupitia kwa mtangazaji wa redio hiyo anaitwa Bonge, yeye ni mtakasaji na amefanya kazi hiyo kwa zaidi ya miaka mitano...!!!??

Sasa naomba tujadili haya na hili lifanywe vipi?

  • Share:

You Might Also Like

0 comments