Mkurugenzi
Ukuzaji Sanaa na Masoko Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Vivian Msao
Shalua (Katikati) akiongea katika halfa ya kumpongeza mwakilishi wa
Tanzania kwenye mashindano ya Airtel Trace Music Stars Afrika kwa
kuibuka mshindi wa mashindano hayo na kuiwakilisha vyema Tanzania .
halfa hiyo ilifanyika katika ofisi za BASATA Ilala Dar es Saalam.
kushoto ni meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando.
Mkurugenzi
Ukuzaji Sanaa na Masoko Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Vivian Msao
Shalua (kulia)akipokea tuzo aliyoipata Nalimi Mayunga mara baada ya
kuibuka mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Afrika. Shughuli hii
imefanyika jana katika halfa ya kumpongeza Mayunga kwa kuiwakilisha
vyema Tanzania katika mashindano ya Airtel Trace Music Stars
iliyofanyika katika ofisi za BASATA. Akishuhudia kushoto ni meneja
uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando.
Baraza
la sanaa Tanzania BASATA leo limempongeza mwakiliwa wa Tanzania katika
mashindano ya Airtel Trace kufatia ushindi alioupata katika mashindano
ya muziki yaliyoshirikisha washiriki 13 toka nchi za Afrika .
Mwisho
mwa mwezi wa tatu BASATA ilimkabidh bendera Mayunga na kumpa kibali cha
kwenda kushiriki mashindano hayo yaliyokuwa yanafanyika nchini Kenya
na kumtakia kila laheri katika mashindano hayo ambapo mwakilishi huyu
aliweza kufanya vizuri na kuibuka kuwa mshindi wa Airtel Trace Music
Star wa Afrika
Mkurugenzi
Ukuzaji Sanaa na Masoko Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Vivian Msao
Shalua katika halfa fupi ya pongezi kwa Nalimi Mayunga katika ofisi za
BASATA alisema” Ushindi huu ni furaha kubwa kwetu sisi Baraza la Sanaa
la Tanzania kwani tunayo dhamana ya kuhakikisha tunaendeleza sanaa
nchini kwa tunashirikiana na wadau mbalimbali nchini katika kuwawezesha
vijana wenye vipaji kukuza sanaa zao ndani na nje ya nchi.
Nachukua
fulsa hii kwa niaba ya BASATA kumpongeza Mwakilishi wetu Nalimi Mayunga
kwa kufanya vizuri na kushinda mashindano haya.
Nawashukuru
sana Airtel kwa kufata taratibu stahiki na kushirikisha BASATA tangu
mashindano haya yaanze ikiwa ni kusajili kampuni yao na kupata hati ya
kufanya shughuli za sanaa na pia kutushirikisha katika mchakato mzima wa
mashindano haya na kumleta mshindi huyu kuchukua hati maalumu ya
kusafiri na kuagwa rasmi wakati wa kuondoka kwenda kwenye mashindano ya
Afrika. Kwakweli huu ni mfano wa kuigwa na wadau wengi na wasanii kwa
ujumla, kufata taratibu na kupata vibali maalumu pindi wanapoenda nje ya
nchi kufanya shughuli za sanaa na kuwakilsisha nchi yetu.
Natoa
wito kwa watanzania kujitokeza kwa wingi pindi awamu ya msimu wa pili wa
mashindano haya ya Airtel Trace yatakapotangazwa ili nao waweze kupata
nafasi ya kushiriki na kuinua vipaji vyao. Aliongea Shalua
Akiongea
kwa niaba ya Airtel Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando
alisema Tunawashukuru watanzania wote walioshiriki katika shindano hili
tangu tulipolizindua. tunampongeza sana mayunga kwa ushindi huu.
Nalimi
Mayunga ameweza kujishindia dili la kwenda marekani na kupata mafunzo
chini ya usimamizi wa Akon,na pia kuweza kurekodi wimbo na video yake ya
kwanza vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya dola za kimarekai 500,000/=
Tunategemea baada ya mafunzo hayo na kutoa wimbo wake na Akon basi
mayunga ataendelea kufanya vizuri na hatimae kuweza kuzifikia ndoto
zake.
Airtel
ilimkabithi Mayunga zawadi ya shilingi million 50 za kitanzania kufatia
ushindi wake hapa nchini na sasa anajiandaa kwenda marekani na kufanya
kazi na msaani nguli Akon.
Akiongelea
ushindi wake Mayunga alisema, nawashukuru sana watanzania kwa kunipigia
kura toka mashindano haya yaanze, najisikia furaha kupata nafasi hii ya
pekee na naamini safari yangu nchini marekani itakuwa ya mafanikio
makubwa na mwanzo wa mafanikio katika kuzifika ndoto zangu za kuwa
mwanamuziki nyota ndani na nje ya nchi.
Nawashukuru
Airtel kwa kuanzisha mashindano haya na BASATA kwa kunipa ushirikiano
wakati wote wa mashindano. Natoa wito kwa watanzania na vijana wenzangu
kuchangamkia fulsa hii pindi msimu wa pili wa mashindano haya
yatakapotangazwa na kuanza .
Mashindano
ya Afrika yalimalizika kwa mtanzania kushika nafasi ya kwanza ,
Nigeria nafasi ya pili na Congo Brazavile nafasi ya tatu.
0 comments