Mcheza
kikapu ‘Hasheem Thabit’ raia wa Tanzania ambaye anachezea timu ya
Oklahoma City Thunder inayoshiriki ligi kuu ya mpira wa kikapu nchini
Marekani maarufu kama NBA amejikuta akitumikia adhabu aliyopewa na timu
yake hiyo ya kutocheza mechi moja na kukatwa mshahara wake baada ya
kumpiga kichwa mchezaji mwenzake wa timu ya New Orleans ‘Greg Stiemsma’
katika mchezo uliozikutanisha timu hizo mbili mwishoni mwa wiki ambapo
New Orleans iliibuka na ushindi wa jumla ya vikapu 105 kwa 102 dhidi ya
Thunder.
Kwa mujibu wa taarifa zinasema
kwamba ikiwa zimebakia dakika takribani 26 kuweza kumalizika kwa kipindi
cha kwanza, Timu anayochezea Thabit ya Thunder ilikuwa inaongoza kwa
vikapu 54 kwa 51 dhid ya Orleans, Thabit alijaribu kumkaba ‘Stiemsma’
hali iliyozua ugomvi baina ya wachezaji hao wawili na kuanza kupigana
vikumbo hali iliyopelekea Hasheem Thabit kumpiga kichwa mlinzi wa kati
wa New Orleans ‘Greg Stiemsma’ na muamuzi wa mchezo huo kupuliza kipenga
kuashiria kusimamisha mchezo na kutoa foul kwa timu hizo huku
akiwaamuru wachezaji hao kuendelea na mchezo.
Katika mchezo huo Hasheem Thabit
aliweza kushinda Point 2 na rebounds 3 ndani ya dakika 14 alizocheza,
hii sio mara ya kwanza kwa Hasheem Thabit kugombana na wachezaji wenzake
kwani kipindi cha nyuma aliwahi kurushiana maneno na kutaka kupigana na
mchezaji wa timu ya Houston Rockets ‘James Harden’.
Kwa wasiomfahamu Hasheem Thabit
ndiye mchezaji anayeongoza kwa urefu katika ligi kuu ya mpira wa kikapu
Marekani ya NBA, anakadiriwa kuwa na urefu wa Futi 7.3 ambazo ni sawa na
mita 2.21 na pia ni raia kutoka Tanzania. Kwa hisani ya vijimambo Blog
0 comments