WASANII WAKALI KUSHIRIKI SHOO YA NGUVU NDANI YA UKUMBI WA DAR LIVE JUMAPILI HII JIJINI DAR ES SALAAM

By Gadiola Emanuel - 3:53:00 PM

Ambwene Yessayah ‘AY’ akiumwagia sifa ukumbi wa Dar Live ambao baada ya kuuona aligundua kuwa una hadhi ya kimataifa.
Meneja wa Kundi la TMK Wanaume Family, Said Fella akithibitisha kundi lake kutoa burudani katika onesho hilo.
Mwana FA akielezea jinsi atakavyofanya makamuzi ya nguvu.
Chegge akielezea jinsi atakavyofunika katika shoo hiyo 'bab kubwa'.
Sehemu ya wanahabari,akiwemo Jane John akisikiliza kwa makini na wadau wengine kwenye mkutano huo.
WASANII wakali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Mwana FA, AY, Kundi la TMK Wanaume Family na Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ kwa pamoja wanatarajiwa kuangusha bonge la shoo siku ya Jumapili hii ndani ya Ukumbi wa Dar Live jijini Dar es Salaam huko Mbagala. 
Akizungumza na wanahabari mchana huu, mratibu wa burudani katika ukumbi huo, Juma Mbizo, alisema maandalizi yote kuhusiana na tamasha hilo yamekamilika.
Picha na Richard Bukos-GPL

  • Share:

You Might Also Like

0 comments