HONGERA ANNE MAKINDA

By Gadiola Emanuel - 6:01:00 AM

Kwa mara ya kwanza katika historia ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Spika wake ni mwanamke. Mwanamke huyo sio mwingine bali ni Mheshimiwa Anna Semamba Makinda. Mheshimiwa Anna Makinda,ametwaa wadhifa huo baada ya kumshinda mpinzani wake, Mabere Marando kutoka CHADEMA.Mheshimiwa Makinda alipata kura 265 dhidi ya kura 55 za Mabere Marando.Jumla ya kura zilizopigwa ni 307 ambapo 9 ziliharibika.Uchaguzi huo umefanyika leo asubuhi mjini Dodoma. Mheshimiwa Makinda ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Njombe Kusini alikuwa ni Naibu Spika katika bunge lililopita ambalo Spika wake alikuwa ni Mh.Samuel Sitta ambaye pamoja na jaribio lake la kugombea tena kuchaguliwa kushika wadhifa huo,wenzake wa CCM waliona ni bora apumzike. ANNA MAKINDA ACHAGULIWA KUWA SPIKA WA KWANZA MWANAMKE:CONGRATULATIONS

  • Share:

You Might Also Like

0 comments