SHINDANO LA KUMSAKA MCHEZAJI BORA WA AFRIKA.BBC

By Gadiola Emanuel - 12:54:00 AM

Hapa tunakuletea maelezo ya kumpigia mchezaji bora wa soka barani Afrika anayetambuliwa na BBC.Baada ya subira ya muda mrefu wakati umewadia kwa kura yako kuamua mchezaji atakayebeba tuzo hiyo kwa mwaka 2008. Ingia hapa kupiga kura kwa kutumia tovuti [internet] Upigaji kura kumpata mchezaji bora wa soka barani Afrika anayetambuliwa na BBC umeaanza Disemba 1 kuanzia saa mbili za Afrika Mashariki au saa moja Afrika ya Kati [1700 GMT majira ya London]. Kura pia zinaweza kupigwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa simu ya mkononi [text au sms].Namba unayotakiwa kutumia ni: +44 77 86 20 20 25. Ingia hapa kupiga kura kwa kutumia tovuti [internet] Kwa wale wanaopendelea kutumia tovuti watatakiwa kuingia katika ukurasa maalum utakaowawezesha kufanya hivyo.Ni lugha ya kiingereza, lakini maelezo yake ni sawa na haya hapa chini. Ili kura yako iweze kutambuliwa na kompyuta unatakiwa kuandika neno "vote" kisha ifuatiwe na: 1 Mohamed Aboutrika 2 Emmanuel Adebayor 3 Didier Drogba 4 Samuel Eto'o 5 Amr Zaki Line za simu za kupigia kura zitafunguliwa tarehe 1 Disemba 2008 na kufungwa tarehe 9 Januari 2009.Mshindi atatangazwa katika wiki inayoanzia tarehe 16 Januari 2009.

  • Share:

You Might Also Like

0 comments