USWAHILI BWANA!!!!

By Gadiola Emanuel - 7:37:00 AM

YANAYO TUFANYA TUWE WASWAHILI... 1.Unamwita mtu usiyemjua(wala kukutana nae kabla)aunt au anco. 2.Asilimia 90 ya CD pamoja na cassete za muziki ulizonazo nyumbani ni feki (sio original copies). 3.Stoo yako imejaa vitu (makorokoro) kwa kuwa hutupi kwa kuamini kuwa ipo siku utayahitaji kwa mfano karpet ukilitoa hulitupi n.k. 4.Una machupa ya maji matupu ya shampoo perfume pamoja na vipodozi vingine umeweka tuu wala huna shughuli navyo. 5.Watoto wako wote wana majina ya utani mfano babu ali,chidi,mamu,dida n.k. 6.Hakuna mtu katika familia yako anayetoa taarifa kwako anapo kuja kukutembelea mfano kaka,shangazi n.k. Sans MS" color=blue size=6> 7.Mifuko yako imejaa vitu kama vile vijiti vya kusafishia meno,tissue n.k ulivyochukua sehemu kama vile mgahawani. 8.Familia yako ina migogoro na ndugu na hawazungumzi kwa muda wa siku 10 au zaidi. 9.Hupigi simu isipokuwa katika muda ambao gharama za kupiga ni nafuu(mfano usiku sana )na mara nyingi huwa una beep tu. 10.Ulipokua mdogo nguo unazonunuliwa pamoja na viatu ni vikubwa mara mbili ili uweze kuvivaa muda mrefu zaidi. 11.Wakati ukisafiri na ndege unabeba mzigo wa uzito mkubwa kuliko inavyoruhusiwa. 12.Unapomsaidia mtu na akafanikiwa basi utakuwa unasema kama sio mimi asingekuwa vile yule. 13. Ualikwapo kwenye sherehe au mkutano hufika baada ya muda ulopangwa kupita waweza zidisha hata masaa mawili mbele au zaidi. 14. unapokuwa kwenye shere hutaki kuchukuliwa moving iwapo kunavideo inayotengenezwa. NOTE. Wapelekee waswahili wengine ili wajue ni kitu gani kinawafanya wao wawe waswahili.......................... kama mimi na wewe , Mmeipata hiyo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Cheers!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  • Share:

You Might Also Like

0 comments