TANZIA :MZEE MUHIDIN GURUMO AMEFARIKI DUNIA

By Gadiola Emanuel - 4:28:00 PM




Marehemu Muhidin Gurumo(kushoto) enzi za uhai wake akiwa na Diamond Platnumz

Mwanamuziki Mkongwe nchini Tanzania, Muhidin Gurumo amefariki dunia jumapili ya tarehe 13/4/2014 majira ya saa nane mchana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa matibabu.

Kwa muda mrefu Mzee Gurumo amekuwa akisumbuliwa na maradhi mpaka siku ya leo alipotangulia mbele ya haki.
Hili ni pengo kubwa katika muziki wa dansi nchini  kwani kwa muda wote wa uhai wake amekuwa akitoa mchango mkubwa katika kuuendeleza muziki huo.

Kifo cha Gurumo kimewagusa wadau mbalimbali wanaopenda na wasiopenda muziki kutokana na umaarufu wake mkubwa aliojingea kupitia kipaji chake kikubwa.
Mtandao huu utaendelea kukupatia taarifa zaidi kadri muda unavyozidi kwenda.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Mzee Gurumo mahala pema. Amen.

  • Share:

You Might Also Like

0 comments