Its all about Launching Kismaty Advert Media Company, advertise with us
By Gadiola Emanuel - 7:24:00 AM
Mkurugenzi wa Kismarty Advert Media Company Ltd Mary Emmanuel ,akisalimiana na viongozi mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo katika uzinduzi wa kampuni ya Matangazo ya Kismaty Advert Media katika ukumbi wa Asili Resort jijini Arusha, Novemba 25 ,2016. |
Wa kwanza kulia ni Meya wa jiji la Arusha Calist Lazaro , mkurugenzi wa Kismarty Advert Media Co. Ltd, Bi. Mary Emmanuel ,na Mratibu wa shughuli hiyo Bi. Dotto Kimaro katika uzinduzi wa kampuni ya Matangazo ya Kismaty Advert Media katika ukumbi wa Asili Resort jijini Arusha, Novemba 25 ,2016. |
Mchekeshaji 'Steve Nyerere' nae hakubakia nyuma alikuwepo akifanya yake katika uzinduzi wa kampuni ya Matangazo ya Kismaty Advert Media katika ukumbi wa Asili Resort jijini Arusha, Novemba 25 ,2016. |
| |||||||||||||
Keki ya ndafu nayo ilihusika sana kwa ukaribu, katika uzinduzi wa kampuni ya Matangazo ya Kismaty Advert Media katika ukumbi wa Asili Resort jijini Arusha, Novemba 25 ,2016. |
Mambo
haya nayo hayakosekaniki katika hafla kama hii shampein ikifunguliwa
hapa na mmoja wa waandishi wa habari wa kituo cha TV jijini Arusha
Millan Cable Hamza Kalemela ,pamoja na mwandishi wa habari kutoka gazeti
la Mwananchi communication Zulfa
Musa katika uzinduzi wa kampuni ya Matangazo ya Kismaty Advert Media katika ukumbi wa Asili Resort jijini
Arusha, Novemba 25 ,2016.Mambo yakiendelea kama uonavyo hapo
pichani,
katika uzinduzi wa kampuni ya Matangazo ya Kismaty Advert Media katika ukumbi wa Asili Resort jijini
Arusha, Novemba 25 ,2016.
|
Na Vero Ignatus wa Wazalendo 25 Blog, Arusha. |
Ameyasema hayo katika uzinduzi wa kampuni ya matangazo inayojulikana kama Kismaty Advert Media company ltd , iliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Asili Resort uliopo Jijini Arusha na kuhudhuriwa na wamiliki wa makampuni mbalimbali hapa nchini.
Meya huyo amewataka wananchi kuwa na tabia ya kutangaza biashara zao kwani bila kufanya hivyo hata kama bidhaa itakuwa na uzuri kiasi gani hakuna atakayefahamu thamani yake bila kuitangaza ndipo ifahamaike.
"Jengeni tabia ya kutangaza biashara zenu na bidhaa mnazokuwa nazo ndugu zangu biashara ni matangazo msikae kimya,ukizingatia hii ni kampuni ya kitanzania,tuache kukuza vya watu tutukuze vya kwetu ndugu zangu "alisema meya.
"Mnapoona kampuni kama hii ya matangazo ndiyo fursa yenyewe hii ya kuitumia kuzitangaza biashara zenu,ukikaa kimya hakuna mtu anayeweza kuifahamu bidhaa yako au biashara yako hata kama unauza vitu vizuri kiasi gani" alisema Meya.
Kwa pande wake mkurugenzi wa Kismaty Advert Media Company ltd ,Bi. Mary Mollel amesema kuwa kampuni hiyo inapokea matangazo ya aina mbalimbali na Kuyasimamia kwa ukaribu na kwa bei ambayo mteja atakayoimudu .
Hivyo amewataka wafanyabiashara biashara mbalimbali kutokuwa waoga kutangaza biashara zao kwani ndiyo njia pekee itakayowasaidia biashara zao kufahamika zaidi na kupata wateja zaidi.
"Msiwe waoga kuthubutu kutangaza biashara zenu hapa tunasaidiana wewe unaleta tangazo nakutangazia kwa bei nzuri na wakati huohuo unapata wateja kwa upande wako ,kwa maana nyingine tunawezeshana karibuni sana. " alisisitiza Bi Mary.