REGENCY INNOVATION SOLUTIONS NA UBA WAZINDUA KADI YA MALIPO YA KIPEKEE AFRIKA JIJINI DAR
By Gadiola Emanuel - 5:02:00 PM
Mkurugenzi
Mkuu wa Regency Innovation Solution, Mike Raymond akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Wakati wa kusaini mkataba
wa maelewano wa kutoa huduma ya kadi ya malipo ya kipekee ya Visa
katika bara zima la Afrika wakianzia nchini Tanzania.
na
uzinduzia kadi mpya ya malipo itakayoitwa Mimosa Black Card, kadi
ambayo itaruhusu mteja kuweka na kutoa fedha bila ya kuhitaji akaunti ya
benki.
amesema
kuwa Kadi hii mpya ni sawa na kadi ya kawaida ya malipo ya kabla ila ni
ya kipekee kwa sababu haiunganishwi na akaunti ya benki hivyo kuifanya
kuwa ya gharama nafuu na pia urahisi wa kuweka na kutoa fedha. Kadi hii
pia italindwa kwa neno la siri (PIN) na teknolojia ya juu ya ulinzi.
Watumiaji
wa kadi ya Mimosa wanaweza kutoa fedha katika mashine za kutolea fedha
(ATM), kufanya malipo ya kutumia kadi katika maeneo yote yenye huduma
hiyo na pia kufanya manunuzi mtandaoni mahali popote duniani kupitia
mtandao wa Visa. Vile vile wateja wanaweza kuweka pesa katika kadi zao
kupitia tawi lolote la UBA Tanzania au mitandao ya simu M-pesa, Tigo
Pesa, Airtel Money na pia katika akaunti za kukusanya fedha katika benki
za CRDB na Exim.
Mkuu
wa Kitengo cha Huduma za Fedha za Kielektroniki wa UBA Tanzania, Tesha
Philemon akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
leoamesema kuwa “ Lengo letu kuu ni kubadilisha mfumo wa jinsi watu
wanavyotumia huduma za kibenki haswa kwa kujikita katika kundi la wale
ambao hawatumii huduma za benki kwa kupitia teknolojia kama hizi.
amesema kuwa ushirikiano wao na Regency Innovation Solutions
utafanikisha lengo kwa kuwafikia wale wasiotumia huduma za benki na
kuwajumuisha katika huduma hizi katika Tanzania na bara la Afrika.
Baadhi ya washiriki katika mkutano huo.
Mkurugenzi wa Mradi wa MIMOSA CONCIERGE, Nassor Sued akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Fedha za Kielektroniki wa UBA Tanzania, Tesha Philemon wa pili kulia na Mkurugenzi Mkuu wa Regency Innovation Solution, Mike Raymond wa pili kudhoto wakiwakisaini mikataba leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Fedha za Kielektroniki wa UBA Tanzania, Tesha Philemon na Mkurugenzi Mkuu wa Regency Innovation Solution, Mike Raymond wakibadilishana mikataba leo jijini Dar es Salaam.